Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte ameapa kusimamisha kile
alichokiita ''siasa potofu za kuhamasisha hisia za umma''. Akizungumza
katika mdahalo kwa njia ya televisheni kabla ya uchaguzi muhimu wa kesho
Jumatano, Rutte ameutahadharisha umma wa waholanzi dhidi ya kumchagua
mpinzani wake, Geert Wilders mwenye msimamo mkali dhidi ya Uislamu,
akisema kuiondoa Uholanzi ndani ya Umoja wa Ulaya kutakuwa na gharama
kubwa sana kwa nchi hiyo. Katika mdahalo huo, Wilders amehimiza msimamo
mkali zaidi dhidi ya Uturuki, akisema Uholanzi inapaswa kumtimua balozi
wa Uturuki.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment