Washambuliaji watatu wa kujitoa muhanga, wanaoshukiwa kuwa wanachama
wa kundi la kigaidi la Boko Haramu waliripua vifaa vya miripuko
walivyokuwa wamejizungushia kwenye miili yao usiku wa Jumamosi mjini
Maiduguri, Nigeria. Watu wasiopungua wanne waliuawa - mmoja wao akiwa
mwanachama wa kundi la ulinzi wa kiraia, na pia mwanamke na watoto
wawili. Maafisa wamesema watu wengine wanane walijeruhiwa. Washambuliaji
walikuwa mwanaume na wasichana wawili wanaoaminika kulifanyia kazi
kundi la Boko Haram. Washambuliaji hao waliingia Maiduguri kwa kunyata
nyakati za usiku, lakini waligunduliwa na wanachama wa kundi la ulinzi
wa kiraia waliokuwa zamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment