Vipimo vya damu vimeonyesha kuwa mfuasi wa itikadi kali alikula
madawa na ulevi kabla ya kuzusha vurugu zilizomalizika wakati
alipomshika mateka mwanajeshi wa kike katika uwanja wa ndege wa Orly
mjini Paris, na kisha kupigwa risasi na kuuawa na wanajeshi wengine
waliokuwa kwenye doria pamoja na mateka. Ofisi ya mwendesha mashitaka wa
jiji la Paris ilisema vipimo vilivyofanywa kama sehemu ya uchunguzi wa
maiti vimegundua dalili za dawa aina ya cocaine na bangi katika damu ya
mshukiwa huyo Ziyed Ben Belgacem. Pia alikutwa na gramu 0.93 za ulevi
katika kila lita moja ya damu wakati alipokufa. Kiasi hicho ni karibu
mara mbili ya kiwango kinachoruhusiwa kwa madereva nchini Ufaransa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment