Kiasi ya watu sita wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa katika
shambulizi la kujitoa muhanga nchini Somalia. Afisa wa Polisi, kapteni
Mohamed Hussein amesema mshambuliaji amejiripua ndani ya gari leo
asubuhi, karibu na hotel ya Weheliye iliyoko kwenye barabara inayotumika
sana ya Maka Almukarramah. Hakuna mtu yeyote ambaye amedai kuhusika na
shambulizi hilo, ingawa mara kwa mara kundi la Al-Shabaab limekuwa
likifanya mashambulizi kama hayo. Hayo yanajiri wakati ambapo mamia ya
wanajeshi wa Somalia jana waliandamana kwenye mji mkuu wa Somalia,
Mogadishu wakilalamika kutolipwa mishahara. Wanajeshi hao ambao wamesema
hawajalipwa mishahara yao kwa zaidi ya mwaka mmoja, walizingira
barabara na kuamuru kufungwa kwa maduka na migahawa. Rais wa Somalia,
Mohamed Abdullahi Farmajo, ambaye amechukua madaraka mwezi uliopita,
aliahidi wakati wa kampeni yake ya uchaguzi, kulishughulikia tatizo hilo
la mishahara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment