Wafanyakazi katika viwanja viwili vya ndege mjini Berlin wamesema leo
kuwa wataendelea na mgomo wao kudai nyongeza ya malipo. Mgomo huo
umesababisha kufutwa kwa karibu safari zote za ndege kutoka kwenye mji
huo mkuu wa Ujerumani. Chama cha wafanyakazi, Verdi kilisema jana kuwa
kitaitisha mgomo wa wafanyakazi katika viwanja vya ndege, siku mbili tu
baada ya mgomo wao wa mwisho siku ya Ijumaa. Mgomo huo uliopangwa kuanza
leo saa 12 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, utamalizika Jumatano
asubuhi na utaathiri kiasi ya safari 660 za ndege. Mratibu wa viwanja
vya ndege, Daniel Tolksdorf, amesema kiasi ya safari 195 za ndege
zilifutwa katika uwanja wa ndege wa Schoenefeld, huku safari 465
zikifutwa katika uwanja wa ndege wa Tegel. Tolksdorf amewataka abiria
kuwasiliana na mashirika ya ndege na kujua iwapo ndege hizo zinaendelea
na safari au la. Verdi inataka nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi
2,000 wa Berlin.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment