Watu wasiopungua 42 wameuwawa kutokana na mashambulio yaliyofanywa na
ndege za kivita kwenye msikiti wa kijiji cha Al- Jineh kilichopo
kaskazini mwa Syria. Taarifa hiyo imetolewa na shirika la haki za
binadamu la Syria lenye makao yake nchini Uingereza. Mkuu wa Shirika
hilo Rami Abdel Rahman amesema ndege ambazo hazikutambuliwa ziliulenga
msikiti huo katika jimbo la Aleppo wakati wa sala ya jioni hapo jana.
Mkuu huyo ameeleza kuwa watu zaidi ya 100 walijeruhiwa katika
mashambulio hayo na kwamba watu wengine wengi bado wamenaswa chini ya
jengo la msikiti huo uliosambaratika. Kijiji hicho kinashikiliwa na
waasi pamoja na makundi ya Waislamu wenye itikadi kali.
Friday, March 17, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment