Rais wa Marekani Donald Trump amewasilisha mswaada wa bajeti yake ya
kwanza inayoweka kipaumbele katika ulinzi. Trump anataka kukata fedha za
wizara ya mambo ya nje. Bajeti ya ulinzi itaongezwa kwa kiasi cha dola
bilioni 54. Fedha kwa ajili ya idara ya ulinzi wa mazingira zitapunguzwa
kwa asilimia 31, wakati bajeti kwa ajili wizara ya mambo ya nje
itapunguzwa kwa asilimia 28. Rais Trump pia anataka kukata kabisa fedha
zinazotolewa na Marekani kwa ajili ya mipango ya ulinzi wa mazingira ya
Umoja wa Mataifa. Hata hivyo hakuna matumaini makubwa ya bajeti hiyo
kukubaliwa na bunge.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment