![]() |
Mkurugenzi Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka |
Na Henry Kilasila
Mkurugenzi
Mtendaji TANESCO, Dkt. Tito E. Mwinuka amesema zoezi linaloendelea la
kukata umeme kwa wadaiwa sugu ni endelevu na amewataka wadaiwa kulipa
Bili zao hasa katika kipindi hiki cha Siku kuu za Pasaka ili kuepuka
usumbufu wa kusitishiwa Huduma ya Umeme.
Ametoa
tahadhari hiyo, Aprili 10, 2017 Ofisini kwake Ubungo Jijini Dar es
Salaam, aidha aliwashukuru Wateja ambao wameshaanza kilipa malimbikizo
ya madeni yao, na ambao wamewekeana makubaliano ya kulipa madeni kwa
awamu na TANESCO.
Aliongeza fedha Shirika linazowadai Wateja wake zinahitajika sana kuboresha miundombinu ya TANESCO.
Akiwa
katika Mkutano huo na wana Habari, pia aliwataka Wateja na Wananchi
kuwa waangalifu kipindi hiki cha mvua kwani hutokea uharibifu katika
miundombinu ya Shirika kama kuanguka kwa nguzo ama nyaya kukatika na
kuwataka kutoa taarifa TANESCO mara moja.
Aidha
kwa Niaba ya Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti ya TANESCO na Wafanyakazi
amewatakia Wananchi wote Heri ya Sikukuu ya Pasaka.
Mwanzoni
mwa Mwezi Machi 2017, TANESCO ilitoa notisi ya siku kumi na nne kwa
Wadaiwa ambao wamelimbikiza madeni ya umeme ambayo iliisha Machi 22,
2017, ikiwa ni kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania
Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuitaka TANESCO kuwakatia umeme
wadaiwa sugu.
Katika
agizo hilo Mhe. Rais aliitaka TANESCO kukusanya madeni kwenye Taasisi
zote inazozidai za Serikali na Binafsi ili kuliwezesha Shirika hili
kutoa Huduma kwa ufanisi.
SHARE
No comments:
Post a Comment