Mdadisi
Bi. Shinuna Said akichukua damu kwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha Chonyonyo wilaya
ya Karagwe mkoani Kagera hivi karibuni kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo
ya UKIMWI unaofanyika nchi nzima.
NA VERONICA KAZIMOTO WA NBS, BUKOBA
IMEELEZWA kuwa asilimia 97 ya watanzania wanaoishi katika
kaya zilizochaguliwa kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI katika
mikoa 11 ambayo imeshafikiwa hadi sasa, wameshiriki kikamilifu katika utafiti huo unaoendelea
kufanyika nchini.
Hayo yamesemwa hivi karibuni na Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi
ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa wakati akitoa taarifa ya
utekelezaji wa utafiti huo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura
Sabora alipofanya ziara mkoani humo kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo
linavyoendelea.
"Ninayo furaha kukutaarifu kwamba,mpaka sasa utafiti
huu umeshafanyika katika mikoa 11ya Tanzania Bara pamoja na visiwa vyote vya
Zanzibar yaani Pemba na Unguja. Jambo la kufurahisha zaidi ni mwitikio wa
wananchi ambao ni asilimia 97 ya wanaoishi katika kaya zilizochaguliwa kwa
ajili ya utafiti kukubali kushiriki," amesema Dkt. Chuwa.
Mikoa ambayo imekamilisha utafiti huu wa Viashiria na
Matokeo ya UKIMWI ni pamoja na Singida, Dodoma, Manyara, Iringa, Njombe na
Ruvuma. Mikoa mingine ni Mbeya, Songwe, Katavi, Tabora na Kigoma.
Nae Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Wambura Sabora
amemwambia Mkurugenzi Mkuu wa NBS kwamba, zoezi la utafiti huo mkoani humo
linaendelea vizuri na mpaka sasa hakuna tatizo lolote lililoripotiwa ofisisini
kwake.
"Nami nichukue fursa hii kukueleza kwamba zoezi hili
linaendelea vizuri hapa mkoani Kagera na mpaka sasa hakuna shida yoyote
iliyojitokeza. Aidha, maeneo ya Kerwa, Missenyi na Wilaya ya Bukoba tayari
yamekamilisha utafiti huu", amesema Sabora.
Kwa upande wake mmoja wa wakazi wa kijiji cha Chonyonyo wilaya
ya Karagwe mkoani Kagera aliyehojiwa na Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina
Chuwa kuhusu jinsi alivyoshiriki kwenye utafiti huo,
alisema amefurahishwa na utafiti huo kwa kuwa amepata fursa ya kupima vipimo
mbalimbali ambavyo hakutarajia kuvipata vyote kwa wakati mmoja.
"Kwakweli nimefurahishwa na utafiti huu kwakuwa
sikutarajia kupima vipimo vya magonjwa ya Homa ya Ini, Kaswende pamoja na
UKIMWI kwa wakati mmoja nikiwa nyumbani kwangu," ameeleza Mkazi huyo wa kijiji
cha Chonyonyo.
Utafiti huu wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania unaendeshwa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania Bara, Wizara ya Afya
kwa Tanzania Zanzibar, Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar (OCGS),
Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS) na Tume ya UKIMWI Zanzibar (ZAC).
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa akimuhoji mmoja wa wakazi
wa kijiji cha Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera kuhusu jinsi zoezi la
Utafiti wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI
lilivyofanyika katika kaya yake. Mahojiano hayo yamefanyika wakati Mkurugenzi
Mkuu huyo wa NBS alipofanya ziara mkoani humo hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi
la utafiti huo linavyoendelea.
Dkt. Chuwa akizungumza baada ya ziara yake
Mkurugenzi
Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa (katikati) akiwa na Muwakilishi
wa Mkurugenzi Mkaziwa Kituo cha Kukinga na Kuzuia Magonjwa, (CDC) Dkt. Eunice
Mmari,(kulia) wakipokea maelezo kutoka kwa mmoja wa wadadisi wanaofanya Utafiti
wa Viashiria na Matokeo ya UKIMWI Bw. John Mark Obura wakati wa ziara iliyofanyika
mkoani Kagera hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.
Mkurugenzi
Mkuuwa OfisiyaTaifa ya Takwimu, (NBS) Dkt. AlbinaChuwa (kulia) akiwa na Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la ICAP Tanzania, Dkt. Fernando Morales (katikati) pamoja na Muwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Kituo cha Kukinga na Kuzuia Magonjwa Tanzania (CDC) cha Marekani,
Dkt. Eunice Mmari (kushoto) wakiangalia jinsi Mdadisi Bi. Shinuna Said
(hayupopichani) anavyochukua damu kutoka kwa mmoja wa wakazi wa kijiji cha
Chonyonyo wilaya ya Karagwe mkoaniKagera hivi karibuni kwa ajili ya Utafiti wa Viashiria
na Matokeo ya UKIMWI wakati wa ziara iliyofanyika
mkoani humo kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.
Mdadisi
Bw. John Mark Obura akihojiwa na baadhi ya waandishi wa habari kuhusu jinsi zoezi
la UtafitiwaViashiria na matokeo ya UKIMWI linavyofanyika mkoani Kagera wakati wa
ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa yaTakwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa iliyofanyika
hivi karibuni kuangalia jinsi zoezi la utafiti huo linavyoendelea.
SHARE
No comments:
Post a Comment