Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa
mazungumzo mapya kuhusiana na mzozo wa muda mrefu wa Sahara magharibi ,
akisema majadiliano yanapaswa kujumuisha mapendekezo kutoka Morocco na
kundi linalodai uhuru la Polisario.
Kwa mujibu wa waraka wa Umoja wa Mataifa , wito wa kuanza tena kwa mazungumzo unakuja baada ya miezi kadhaa ya hali ya wasi wasi katika jimbo hilo linalogombaniwa , ambalo Morocco inadai kuwa sehemu ya taifa hilo la Kifalme na chama cha Polisario kinasema eneo hilo ni mali ya watu wa Saharawi ambao walipigana vita vya chini kwa chini hadi makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyosimamiwa na Umoja wa mataifa mwaka 1991.
Juhudi za Umoja wa Mataifa kufikia suluhisho la mzozo huo zimeshindwa kwa miaka kadhaa katika eneo hilo ambalo sehemu kubwa ni jangwa.

No comments:
Post a Comment