Rais wa Marekani, Donald Trump ameendelea na mipango ya kuiuzia
Nigeria ndege kadhaa za kivita katika mapambano yake dhidi ya kundi la
itikadi kali la Boko Haram, ambalo limesababisha mtafaruku katika taifa
hilo lenye wakaazi wengi barani Afrika kwa mashambulio ya mabomu na
mauaji.
Makubaliano hayo , ambayo hapo awali yalikubaliwa chini ya utawala wa rais wa zamani Barack Obama, yalicheleweshwa baada ya jeshi la anga la Nigeria kushambulia kituo cha wakimbizi , na kuuwa zaidi ya raia 90.
Vyanzo katika bunge la Marekani Congress vimewaambia waandishi habari kwamba hali ya wasi wasi bado inaendelea kuwapo juu ya iwapo serikali ya Nigeria itaweza kulipia gharama kamili za ndege hizo mbazo ni dola milioni 600.

No comments:
Post a Comment