Leo ni siku ya
maadhimisho ya ungojwa wa malaria duniani , nchini Jamhuri ya
kidemokrasia ya kongo, changa moto bado ni kubwa katika kuutokomeza
ugonjwa huo kama ambavyo malengo ya shirika la afya duniani WHO lilivyo
la kumaliza ungojwa huo mpaka ifikapo mwaka 2030.
MBU
Chanjo ya kwanza ya malaria duniani itajaribiwa kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka ujao.
Shirika la Afya Duniani WHO limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu ya maisha, huku malari ikiendelea kupoteza maisha ya watu.Mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi ya watoto laki saba wenye umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na nusu.
Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia mia moja, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.
Hii inafuata miongo kadhaa ya tafiti ya kutafuta ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo duniani.
Chanjo hiyo mpya, itakwenda sambamba na hatua nyengine za kujikinga kama vile neti, dawa za kufukuza mbu, na dawa za kukinga malaria.
Wakati wa majaribio, maelfu ya watoto watapewa chanjo hiyo mara nne katika kipindi cha miaka miwili.
SHARE
No comments:
Post a Comment