Mkuu
wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, akiongozana na Waziri wa
Nchi POfisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu, Bunge na Watu Wenye
Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama wakikagua maandalizi ya mwisho mwisho ya
maadhimisho ya Sherehe za Miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
kwenye uwanja ya Jamhuri mjini Dodoma. Maadhimisho hayo yataongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Jumatano Aprili 26, 2017.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya
maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya
maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Vikosi
vya Ulinzi na Usalama vikiwa kwenye gwaride la maandalizi ya
maadhimisho ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar yanayotarajiwa kufanyika terehe 26 Aprili Mjini Dodoma.
Askari wa Pikikipi maalum wakionesha namna pikipiki hizo zitakavyopamba maonesho hayo.
Makomandoo
wa Jeshi la wananchi wa Tanzania wakionesha umahiri wao wa kuvuta gari
lenye tani 7 ikiwa ni moja ya mbinu ya medani katika uwanja wa
mapambano.
Askari wa Kikosi cha Farasi wakionesha umahiri wao katika kutumia farasi kupambana na uhalifu.
Wanafunzi wa halaiki wakipita kwa ukakamavu mbele ya Jukwaa Kuu.
NA IMMACULATE MAKILIKA- MAELEZO – DODOMA
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Ajira na Wenye
ulemavu, Jenista Mhagama amewaasa Watanzania kuwa wazalendo pamoja na
kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.
Akizungumza,
leo mjini Dodoma wakati akifuatatilia maandalizi ya Maadhimisho ya
miaka 53 ya Muungano yatakayofanyika Aprili 26 mwaka huu katika Uwanja
wa Jamhuri uliopo mjini Dodoma.
“Tunapoadhimisha
miaka 53 ya Muungano ninawaomba watanzania kuwa wazalendo pamoja na
kulinda amani ya nchi” alisema Waziri Mhagama Pia, Waziri Mhagama
aliwaomba watanzania hasa wakazi wa Dodoma kuhudhuria kwa wingi katika
Maadhimisho hayo yatakayofanyika jumatano wiki hii. Kwa upande wake,
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema kuwa mkoa wake
umejipanga vizuri katika kufanikisha maadhimisho hayo, ambapo pia
alivishukuru vyombo vya habari kwa kuhamasisha wananchi juu ya
maadhimisho hayo.
“Wananchi
wamehamasika kushiriki katika maadhimisho haya ya miaka 53 ya Muungano,
ninawashukuru kwa kazi kubwa mliyoifanya na tunaamini mtaendelea
kuhamasisha wananchi kushiriki katika maadhimisho hayo” alisema
Rugimbana Maandalizi ya Maadhimisho ya miaka 53 ya Muungano
yamehudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mndeme,
pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Aidha,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, ambapo pia
yatahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohammed Shein na viongozi mbalimbali wa dini na
Serikali. Maadhimisho hayo ya miaka 53 ya Muungano yanatarajiwa kupambwa
namaonesho kutoka kutoka vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama,
burudani za vikundi vya ngoma pamoja na maonesho ya halaiki.
SHARE
No comments:
Post a Comment