Nchini Afrika Kusini hapo jana waandamanji walikusanyika nje ya
wizara ya fedha, kupinga hatua ya kuondolewa kwa Waziri wa Fedha Pravin
Gordhan.
Gordhan mwenye kuheshimika kimataifa aliondolewa Alhamisi jioni
na nafasi yake kuchukuliwa na Malusi Gigaba, ambae aliwahi kuwa waziri
wa mambo ya ndani wa taifa hilo.
Hatua hiyo iliyochukuliwa na Rais Jacob
Zuma imesababisha kuporomoka kwa sarafu ya nchi hiyo ya randi. Katika
hotuba yake kwa Waafrika Kusini iliyooneshwa kwa njia ya televisheni,
Zuma alisema mabadiliko hayo aliyoyafanya yana lengo la kustawisha ubora
na ufanisi.
Aidha, Rais Zuma amebadilisha mawaziri 10 miongoni mwa
mawaziri 35, akiwemo wa nishati, polisi na utalii.
SHARE
No comments:
Post a Comment