TRA

TRA

Saturday, April 1, 2017

Mbio za urais Ufaransa zazidi kuwa ngumu

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
UCHUNGUZI wa maoni uliotolewa leo hii unaonyesha kuwa mchuano wa kinyang'anyiro cha urais nchini Ufaransa unazidi kuwa mgumu tofauti na siku saba zilizopita wakati ambapo zimesalia wiki tatu tu kabla ya kuanza upigaji kura. 

Raundi ya kwanza ya upigaji kura inayowalenga wanaoongoza kwenye kinyang'anyiro hicho Emmanuel Macron wa sera za mrengo wa kati na Marine Le Penn wa sera za mrengo mkali wa kulia kwa pamoja wameanguka kwa asilimia 1, hadi 25 na 24, huku mgombea wa kihafidhina Francois Fillon anayeshika nafasi ya tatu akijiongezea alama 2 na kufikia asilimia 19.

 Jean-Luc Melenchon kutoka mrengo mkali wa kushoto amefikia asilimia 15, baada ya kuongeza alama 1. Ikiashiria kuongezeka kwa sintofahamu, asilimia 38 ya watu ama hawakuweza kusema ni kwa namna gani watapiga kura ama wanaweza kubadilisha maamuzi, ingawa kiwango hicho kimeshuka, lakini bado ni kikubwa kwa viwango vya uchaguzi nchini Ufaransa.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger