Meya wa Jiji
la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwa katika utaratibu wa kuingia ndani ili aweze
kukaguliwa kama abiria wengine wa kawaida tayari kwa safari kuelekea nchini
Iran.
Meya wa Jiji
la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiaga wakati akielekea ndani ya uwanja tayari kwa
safari kuelekea Nchini Iran.
Meya wa Jiji
la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwasiliana na baadhi ya jamaa zake kabla ya
kuondoka uwanjani hapo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam jana jioni tayari kwa safari kuelekea Nchini Iran kwa ziara ya kikazi ya siku kumi.
NA CHRISTINA
MWAGALA, OMJ
Meya wa jiji
la Dar es Salaam Isaya Mwita ,ameondoka Nchini jana kuelekea Iran kwa mualiko
wa ziara ya kikazi ya siku 10 ikiwemo na mkutano wa siku mbili utakaofanyika katika mji wa Bashar.
Aidha Meya
atapata nafasi ya kuzungumza na rais wa Jamhuri ya Kiislamu wa Iran Hassan
Rouhani kabla ya kufanyika kwa mkutano wa siku mbili katika jiji la Bashar
utakao husisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji.
Katika
mkutano huo ambao utahusisha majadiliano mbalimbali kuhusu majiji, ambapo baada
ya mkutano huo ataelekea mjini Teherani
kwa mualiko maalumu wa Meya wa jiji hilo Muhammed Bakir Galbaf ambapo
pamoja na mambo mengine watajadiliana fursa za kibiashara katika majiji hayo
mawili.
Aidha katika
mazungumzo hayo, watajadiliana pia namna ya kutatua changamoto zilizopo kwenye
majiji na namna ambavyo wanaweza kuyatatua.
“ Iran na
Tanzania ni nchi marafiki kwa kipindi kirefu kwahiyo utaona kwamba mambo mengi
wamekuwa wakishirikiana na sisi, kwahiyo ni fursa pia kwa majiji haya mawili
kubadilishana uwezo wa kuendeleza jiji letu, nimechaguliwa na wananchi na wao
wanataka maendeleo “ alisema Meya Isaya.
Aliongeza
kwamba akiwa nchini humo atapata fursa ya kushuhudia kampeni za uchaguzi mkuu
ambapo miongoni mwa wagombea wa nafasi ya urais Meya wa jiji la Teheran ni
mmoja wapo.
“ Kushudia
kwangu kampeni sio kwamba nataka kugombea nafasi ya uras hapa nchini , hapana
ila ni moja ya kujifunza namna ambavyo wenzetu wanafanya kampeni zao”
alifafanua.
Hata hivyo
Meya aliwasi wakazi wa jiji la Dar es Salaam hususani wanaoishi mabondeni
kuchukua tahadhari kwani bado mvua zinaendelea kunyesha na hivyo kujikinga na
mafuriko.
SHARE
No comments:
Post a Comment