ZAIDI
ya miradi 25 inatarajiwa kutekelezwa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Nchini kama sehemu ya kushiriki katika ujenzi wa Uchumi wa viwanda nchini.
Hayo
yalisemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Nchini,
Meshach Bandawe (pichani) wakati alipokuwa akiwasilisha mada ya
ushiriki wa Mifuko ya Hifadhi katika Ujenzi wa uchumi wa Viwanda katika
mkutano wa wanachama na wadau wa Mfuko wa PPF uliofanyika Jijini Arusha hivi
karibuni.Bandawe alisema kuwa Miradi hiyo itahusu viwanda
vitakavyotekelezwa na Mfuko mmoja mmoja pamoja na Viwanda
vitakavyotekelezwa na Mifuko yote kwa pamoja kupitia Umoja wao wa TSSA
(Tanzania Social Security Association).
"Viwanda
hivyo ambavyo vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji, inajumuisha
baadhi ambavyo vimeanza uzalishaji na vingine vipo katika hatua za
kufanyiwa upembuzi yakinifu ambavyo kati ya hivyo vipo ambavyo
vilisimama uzalishaji ambavyo vitahitaji kufufuliwa, vipo ambavyo
vilikuwa vikisuasua katika uzalishaji na uendeshaji ambavyo vitahitaji
kuendelezwa na vingine vitajengwa upya". alisema Bandawe.
Alivitaja
Baadhi ya Viwanda hivyo kuwa ni Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi na
Mbigili, viatu Karange Moshi, Vinu vya NMC Iringa, Dodoma na Mwanza,
Viuadudu Kibaha, General Tyre Arusha, Chai Mponde, Nguru Ranch Morogoro,
Mvinyo na Juisi ya Zabibu Dodoma, Kilimanjaro Machine tools, Tandahimba
na Newala Cashewnut Union, sukari ya sweetner Tanga, Kilimo cha Wanga
Lindi, Kiwanda cha Madawa TPI, Chai Kagera, Morogoro Canvas, Urafiki Dar
es Salaam, Vunu vya kuchambulia pamba vya Nyanza Cooperative Union,
Viwanda vya Ngozi na bidhaa za Ngozi nk.Viwanda hivi ambavyo vina
mnyororo mrefu wa uogezaji thamani vitategemea mali ghafi kutoka ndani
ya Nchi, vitahusu pia bidhaa zinazotumiwa na watu wengi kwa ajili ya
soko la ndani na Nje ya Nchi, vitatengeneza ajira nyingi na hivyo pia
kupanua wigo wa wanachama wengi watakaojiunga na Mifuko hiyo na baadae
kuimarisha uchumi wa Nchi.
Uwekezaji
huu wa viwanda utakuwa wenye tija kwa wanachama, mifuko na taarifa kwa
ujumla na miradi yote itafanyiwa upembuzi yakinifu ili kuhakikisha
usalama wa fedha za wanachama na itafuata kanuni taratibu na miongozo
mbalimbali ya uwekezaji na wataalam watatumika katika hatua mbalimbali
za utekelezaji. Viwanda hivi vitakapokamilika vinategemewa kuzalisha
ajira zaidi ya watu 114,000 Nchini.
Umoja a Mifuko ya Hifadhi unaundwa na Mifuko ya NSSF, PPF, LAPF, PSPF, GEPF, NHIF, WCF na ZSSF uliopo Zanzibar.
SHARE
No comments:
Post a Comment