Makamu wa Rais wa Marekani Mike
Pence na naibu Waziri mkuu wa Japan Taro Aso,wamekubaliana kuweka
msukumo wa Kidiplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kasikazini
kuishinikiza kuachana na mpango wake wa silaha za Nyuklia.
Marekani itaendelea kushirikiana na Japan na washirika wengine katika ukanda na China,kuweka vikwazo vya kidplomasia na kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini,ili iachane na mpango wake wa silaha za nyuklia.Lakini mapendekezo yote yanaendelea kujadiliwa.
Katika mkutano huo Abe amemwambia Pence kuwa Japan inataka kufikia makubaliano kwa njia ya majadiliano.
Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence
"Ukizingatia kwa sasa mazingira ya Korea Kaskazini si mazuri,nafikiri ziara yako kwa wakati huu imekuja wakati muafaka.kimsingi tunatakiwa kuwa na njia ya amani kuhusiana na jambo hili,japo kuwa nafikiri mazungumzo kama mamzungumzo kwa jambo hili halina maana.Ni muhimu kwetu kutumia nguvu dhidi ya Korea Kaskazini kuihusisha katika mazungumzo kwa kina."
Marekani kwa sasa imekuwa ikitafutwa uungwaji mkono katika kuikabili Korea Kaskazini.
SHARE









No comments:
Post a Comment