
Wazungu watatu waliuawa na mwingine
kujeruhiwa vibaya baada ya mtu mweusi mwenye silaha kuanza kufyatulia
watu risasi eneo la Fresno, California nchini Marekani, polisi wamesema.
Mkuu
wa polisi Jerry Dyer amesema Kori Ali Muhammad alifyatua jumla ya
risasi 16 katika muda wa dakika 90 wakati wa shambulio hilo Jumanne.Alikuwa akisema: Mungu ni Mkubwa kwa Kiarabu alipokuwa akikamatwa na polisi.
Maafisa hata hivyo wanaamini kisa hicho kilikuwa cha chuki za ubaguzi wa rangi na si ugaidi.
- Walio na akili punguani kupokonywa bunduki Marekani
- Wanafunzi kuingia na bunduki darasani Texas, Marekani
Mshukiwa huyo alikuwa ameandika kwenye mitandao ya kijamii kwamba anawachukia sana Wazungu na pia akaandika ujumbe ulioashiria kwamba alikuwa anaipinga serikali.
"Alitaka kuua watu wengi na alitaka kutekeleza hilo. Kilikuwa kisa cha ghafla tu cha ghasia. Ni mtu ambaye hakuwa amechokozwa na alikuwa na nia ya kutekeleza mauaji."
Bw Muhammad, ambaye alifahamika sana kwa jina la utani kama Yesu Mweusi sasa anakabiliwa na mashtaka manne ya mauaji na mawili ya kukusudia kuua.
Kisa hicho huenda kikafufua tena mjadala kuhusu haki ya raia kumiliki silaha Marekani.
Watu zaidi ya 30,000 huuawa kwa kupigwa risasi nchini humo kila mwaka.
SHARE








No comments:
Post a Comment