NA MWANDISHI MAALUM
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es
Salaam Aprili 21, 2017, Dimond alisema ameamua kuingia kwenye soko
la kutengeneza pafyum zenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini.
Ameongeza
kwamba kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira
kwa vijana wengi lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia
kodi zitakazotozwa kutokana na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake
wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya CHIBU itapatikana katika maduka yote
ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika
mkakati mwingine wa soko Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes
amesema wako katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la
ndege la Kenya Airways kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha
kwenye soko la kimataifa ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka
makubwa kwenye viwanja vya ndege katika nchi mbalimbali ambako ndege za
shirika hilo zinafika

Mwanamuziki
Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Plutnamz akimkabidhi chupa ya Pafyum
iitwayo "Chibu", Aisha Azori mteja wake wa kwanza aliyenunua bidhaa hiyo
kwenye maduka ya GSM Mall jijini Dar se Salaam lAprili 21, 2017.

Mwanamuziki
Naseeb Abdul maarufu, Diamond Plutnamz akizungumza na waandishi wa
habari wakati akizindua Pafyum hiyo kulia ni Mmoja wa Mameneja wake Babu
Tale.


Meneja
wa Diamond Plutnamz, Salaam Medes akizungumza mara baada ya kuzindua
pafyum hiyo kwenye duka kubwa la GSM Mall barabara ya Nyerere jijini Dar
es salaam.

Diamond akiionyesha pafyum hiyo

Salaam Mendes akitaja bei ya pafyum hiyo kwa waandishi wa habari mara baada ya kuizindua rasmi jijini Dar es salaam.
SHARE
No comments:
Post a Comment