Kaimu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini, Tito Haule (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja wakitia saini mkataba utakaoiwezesha Covenant bank kutoa huduma mbalimbali za bima kwa vyama vya ushirika nchini, waliosimama ni kutoka kushoro ni, Mwanasheria wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Angela Chilewa, Meneja Uendeshaji wa Covenant Bank, Baraka Enock pamoja na Mwanasheria wa Benki hiyo Hadija Sijaona. Aliyeketi ni Kaimu Naibu Mrajisi Udhibiti na Usimamizi, Collins Nyakunga.
KAIMU Mrajisi wa Vyama vya ushirika nchini, Tito Haule amevitaka vyama vyote vya Ushirika nchini kujiepusha kujiingiza kwenye mikopo isiyokuwa na tija kutoka katika taasisi mbalimbali za kifedha, ambayo inavighalimu vyama hivyo na kushindwa kujiendesha kutokana na kuzidiwa na madeni ambayo hayaendani na uwezo halisi wa vyama husika na kuwaingiza wanachama wao katika matatizo kutokana na kushindwa kulipa madeni hayo huku akiwashauri kuangalia huduma ambazo zinawalenga wananchi moja kwa moja.
Kiongozi
huyo ameyasema hayo wakati wa kusaini makubaliano na Benki ya Wanawake ya
Covenant ambayo yataiwezesha benki hiyo kuweza kutoa huduma mbalimbali za bima
pamoja na mafunzo ya ujasiriamali kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini,
Katika hafla hiyo iliyofanyika mkoani Dodoma Mrajisi ameitaka benki hiyo
kuhakikisha inatimiza adhma ya kutoa huduma ambazo zitawanufaisha wanachama
moja kwa moja na sio viongozi wachache.
“Vyama
vingi vimekuwa na mazoea ya kujiingiza katika mikopo mikubwa na wakati mwingine
hata kuzidi uwezo halisi wa vyama husika, lakini pia viongozi wanaokuwepo
wanakuwa sio waaminifu na kujikuta wanashindwa kusimami matumizi ya fedha hizo
kwa uaminifu na kujikuta wanaviingiza vyama katika matatizo makubwa,” alisema Haule
na kuongeza kuwa, “Ninawsaihi viongozi waache utaratibu huu ambao umeendelea
kuvifanya vyama vya ushirika kushindwa kuwa sehemu ya ukombozi wa wanachama
wake bali sehemu ya kuwakandamiza,”
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Covenant Bank, Sabetha Mwambenja,
akizungumza kabla ya kusaini mkataba huo utakao iwezesha benki hiyo kufika
maeneo mbalimbali nchini kutoa huduma kwa vyama mbalimbali vya ushirika nchini
amesema atahakikisha benki yake inafanya kazi waliyokubaliana na msimamizi huyo
wa vyama vya ushirika kwa uaminifu na weledi ili kuweza kuwainua wanachama wa
vyama vya Ushirika.
“Tumefanya
utafiti kwa muda mrefu sasa, kuangalia namna ambavyo tunaweza kuwasaidia
wajasiriamaliwadogo miongoni mwao wakiwemo wakulima, wafugaji, wavuvi pamoja na
wafanya biashara, tumegundua wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo kukosa
huduma za Bima ya matibabu pamoja na ajali, hivyo tumeanzisha huduma hizo ili
kuwaondolea mzigo ambao wanaupata kila siku wanapopata fedha wanashindwa kuweka
akiba,”
Mkurugenzi
huyo alihitimisha kwa kumshukuru mrajisi kuwapatia ruhusa ya kuhudumia vyama
vya Ushirika nchini na kusisitiza kuwa watatoa ushirikiano kwa ofisi hiyo ili
kuhakikisha mamilioni ya wanachama wa vyama vya ushirika wananufaika moja kwa
moja na huduma zitakazo tolewa na benki hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment