TRA

TRA

Tuesday, April 25, 2017

Rais Salva Kiir ashutumiwa na Sudan kwa kuwahifadi waasi

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
SHIRIKA la Ujasusi na Usalama wa Taifa la Sudan limemlaumu Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir kwa kuwapa hifadhi waasi ili kuendeleza vita nchini Sudan. 


                        Rais Salva Kiir

Kwenye tamko lake shirika hilo la ujasusi limeionya serikali ya Sudan Kusini na kuitaka serikali ya nchi hiyo iache mara moja kujiingiza katika mambo ya ndani ya Sudan. 

Mapigano katika mipaka ya pande zote mbili yameharibu uhusiano wa nchi hizo hali ambayo inaonyesha dalili ya mvutano kuendelea kuwa mkubwa baina ya nchi hizo mbili. 

Sudan ya Kusini ilijitenga na Sudan mnamo mwaka 2011 kwa mujibu wa mkataba wa amani uliovimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka 22 katika Sudan.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger