NA VICTOR MASANGU, KIBAHA.
KATIKA
kuunga juhudi za serikali ya awamu ya tano kupambana na wimbi la
umasikini taasisi ya Namelok ya Wilayani Kibaha inatarajia kujenga kituo
maalumu cha wasichana na wanawake wajasiriamali ambacho kitakuwa
kinajihusisha na masuala ya utoaji wa mafunzo mbali mbali kwa lengo la
kuweza kuwapa fursa ya kuachana na kuwa tegemezi na kujiajiri wao
wenyewe.
Akizungumza
katika sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa kituo hicho zilizofanyika
katika Kata ya Mwendapole iliyopo katika halmashauri ya mji wa Kibaha
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Janet Mwasuka amesema kukamilika
kwa ujenzi huo kutaweza kuwa ni mkombozi mkubwa wa kuwainua wanawake
hao kiuchumuni kupitia mafunzo ya stadi za kazi pamoja na fursa
zilizopo kutokana na elimu watakayoipata.
Janet
alibainisha kuwa anatambau kuwa wanawake wegine katika Wilaya ya Kibaha
ambao baadhi yao wameshindwa kutimiza ndoto zao kutokana na kukosa
elimu ya ujasiriamali hivyo ana imani kituo hicho kitaweza kusaidia kwa
kiasi kikubwa kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa wanawake
pamoja na jamii yote kwa ujumla.
Naye
Mkurugenzi wa Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Purple Planet ya Jijini
Dar es Salaam inayojishughulisha na kuwasaidia katika kuendesha
biashara zao na kuwainua kiuchumi wanawake wajasiriamali Hilda Kisoka
amebainisha kuwa mikakati yao waliyojiwekea ni kufika mbali zaidi na
kuuza bidhaa wanazozizalisha hapa nchini hadi nje ya nchi kwa lengo la
kujitangaza zaidi.
Alisema
kwamba ana imani wanawake wengi hapa nchini wana uwezo mkubwa wa
kuengeneza bidhaa zenye ubora wa hali ya juu hivyo ameiomba serikali ya
awamu ya tano kuwasaidi kwa hali na mali ili kuweza kufika mbali katika
kuleta ushindani zaidi wa masoko katika nchi zingine za nje na
kuondokana na kuwa tegemezi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Happiness Seneda ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika uzinduzi huo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
amekemea vitendo vya wanawake kufayiwa vitendo vya ukataili na
unyanyasaji na kujikuta baadhi yao wanashindwa kutimiza ndoto zao na
malengo yao waliyojiwekea katika siku za baadae.
“Jamani
mimi mwenyewe nimeshuhudia baadhi ya maeneo kuna watu wanafanya vitendo
vya ukatili na kuwanyanyasa wanawake yani hili suala kwa upande mimi
kwa kweli silipendi kwa sababu baadhi ya wanawake wanashindwa kutimiza
malengo yao ambayo yamejiwekea kwa hiyi katika hili sisi kama serikali
ni lazima tulivalie njuga ii kuondokana na hali hii,”alisema Seneba
Pia
katika hatua nyingine alitoa wito kwa wakinababa wote katika Mkoa wa
Pwani kuachana na vitendo hivyo vya kuwanyanyasa wanawake na kuwapiga
bila sababu zozote za msingi na badala yake wabadilike na kuhakikisha
kwamba wanawasaidia kuwawezesha katika shughuli zao mbali mbali za
ujasiriamali kwa lengo la kuweza kupambana na wimbi la umasikini.
KITUO
hicho ambacho kinajegwa katika kata ya Mwendapole kinatarajiwa mpaka
kukamilika kwake kugharimu kiasi cha shilingi milioni 45 na katika
awamu ya kwanza kinatarajia kuwanufaisha wanawake wapatao 200 kutoka
Wilayani Kibaha mkoani Pwani pamoja na maeneo mengine ya jirani ambao
watapatiwa mafunzo mbali mbali ya ujasiriamali.
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe kulia Happiness Seneda akionyeshwa eneo lililopo
kata ya Mwendapole na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Namelok Janet
Mwasuka wa kushoto ambapo kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili
ya wasicahna na wanawake wajasiriamali waliopo Wilayani Kibaha Mkoani
Pwani (PICHA NA VICTOR MASANGU)
Mkuu
wa Wilaya ya Kisarawe (kulia) Happiness Seneda kulia akiwa amemshika
mmoja wa watoto huku akisikiliza maelekezo kuhusina na ujezni wa kituo
hicho maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichan na wakinamama
kinachijengwa katika kata ya Mwendapole Wilayani Kibaha. Kushoto kwake
ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Namelok, Janet Mwasuka.
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Nameloc akoinyesha eneo ambalo
kutajengwa kituo maalumu cha elimu kwa ajili ya wasichana na wanawake
wajasiriamali katika kata ya Mwendapole Wilayani Kibaha Mkoani Pwani
SHARE
No comments:
Post a Comment