NA HUSNA
SAIDI NA NURU JUMA- MAELEZO
MAMLAKA ya
Mapato Tanzania (TRA) imekusanya Trilioni 10.87 mpaka kufikia Machi mwaka huu
kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Hayo yamesemwa
na Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Charles Edward Kichere wakati wa mahojiano na mtangazaji wa TBC1
Rashid Salum katika kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa kila siku za Jumatatu saa moja
kamili jioni na Alhamisi saa tatu na nusu usiku.
Kichere alisema,
mwaka huu wa fedha 2016/2017 TRA inatakiwa kukusanya Trilioni 15.105 na hadi
kufikia Machi mwaka huu TRA imefanikiwa
kukusanya Shilingi Trilioni 10.87.
Aliendelea kwa
kusema kuwa mpaka kufikia Juni mwaka huu TRA itahakikisha inatimiza lengo la
kukusanya Shilingi Trilioni 15.105 ili kusaidia Serikali kuleta maendeleo kwa wananchi
wake.
Alisema kuwa TRA
ina waajiriwa wapya ambao wamepewa mafuzo ya miezi sita katika chuo cha
kodi juu ya mifumo mbalimbali ya ukusanyaji kodi ambao waliajiriwa moja kwa
moja na mamlaka hiyo kwaajili
ya kutekeleza majukumu ya ukusanyaji kodi ndani ya nchi.
“Tunatumia mfumo
wa Tehama kukusanya kodi na mifumo mingine mbalimbasli kama vile Tigo Pesa , Airtel
Money na MPesa ili kurahisishia watu kulipa kodi wakiwa nyumbani na kuepuka
usumbufu,” alisema Kichere.
Kichere
aliongeza kuwa kwa mwaka huu wa fedha mapato yameongezeka mpaka kufikia
asilimia 9.9 hadi 10 licha ya kuwa kuna baadhi ya maeneo hawakuweza kukusanya.
Aidha Kichere
alisema Mamlaka kwa sasa imejipanga kuwa na mahusiano mazuri na wafanyabiashara
ili kuhakikisha wafanyabiashara wanalipa kodi stahiki na kwa mujibu wa sheria
bila kutumia nguvu au uonevu wowote.
Hata hivyo
mamlaka hiyo imekuwa ikitoa elimu
kwa walipa kodi kwa kupitia vyombo mbalimbali vya habari, kutoa semina kwa
watumishi wa umma , kuandaa makongamano ambayo yanatoa elimu, kupitia mitandao
ya kijamii na ziara mbalimbali ambazo wamekuwa wakizifanya ili kuhakikisha
wafanyabiashara wanapata elimu pamoja na kujua wajibu wao katika kulipa kodi
ili kuleat maendeleo nchini.
No comments:
Post a Comment