TRA

TRA

Tuesday, April 25, 2017

Trump na Merkel waijadili Korea Kaskazini

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais wa Marekani Donald Trump na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel walijadiliana kwa njia ya simu juu ya Korea Kaskazini. 

Kwa mujibu wa Ikulu ya Marekani, viongozi hao walitilia maanani hatari kubwa ya usalama inayosababishwa na Korea Kaskazini. 

Viongozi hao pia walijadili juu ya migogoro ya Syria, Yemen na Mashariki mwa Ukraine. Rais Trump alisisitiza msimamo wa nchi yake wa kuziunga mkono juhudi za Ujerumani katika kufanya mazungumzo ya kuleta suluhisho la amani juu ya mgogoro wa nchini Ukraine. 

                                          Angela Merkel

Na wakati huo huo, Rais Trump ameutaka Umoja wa Mataifa ufanye mageuzi makubwa na kulilaumu shirika hilo kwa jinsi linavyo yashughuklikia maswala ya dunia.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger