Mgombea urais
nchini Ufaransa Emmanuel Macron ameshinda duru ya kwanza ya uchaguzi wa
nchi hiyo, huku dalili zikionyesha, baada ya wiki mbili atapambana
katika duru ya pili na Marine le Pen ambae ni mgombea wa chama chenye
mrengo wa kulia cha National Front. Aboubakar Famau na taarifa zaidi:
"Nimesikia katika miezi iliyopita na leo tena, shaka, hasira na uoga waliokuwa nao wafaransa. Na hamu ya mabadiliko. Hiki ndicho kilichowasukuma kuacha vyama vikuu viwili vilivyotawala kwa zaidi ya miaka thelathini.")
Ameongeza kusema kazi yake hivi sasa ni kuipatanisha nchi na kuunganisha nguvu kwa ajili ya duru ya pili ya uchaguzi."wiki mbili kuanzia sasa, nataka niwe rais wenu. (CROWD CHEERING) Rais wa raia wote wa ufaransa. Rais wa wapenda nchi dhidi ya vitisho vya wanaotaka kujitenga.")
Kwa upande wake, Le Pen ameyaelezea matokeo hayo kuwa ni ya kihistoria. Huku akijiita kuwa yeye ni ndio chaguo la wafaransa na kusema kuwa muda umefika wa kuwabadilisha watu.
"Wakati umefika wa kuwaweka huru raia wa ufaransa na jamii yote wa rais wa Ufaransa bila kusahau marafiki zetu walio nje ambao wameniamini na naona fahari kwa imani walioonyesha kwangu.")
Rais wa ufaransa amempigia simu bwana Macron na kumpongeza, bila kuonyesha kumuunga mkono rasmi.
Mmoja wa wasaidizi amesema haikuna vigumu kujua chaguo lake kati ya waziri aliyefanya kazi nae na mwakilishi mwenye mrengo wa kulia.Francois Fillon ambae ni mgombea wa mrengo wa kati, na aliyewahi kuwa waziri mkuu, ambae pia aliwahi kukabiliwa na tuhuma za ufisadi, wakati akiwahutubia wafuasi wake amesema atampigia kura Macron.
Wakati hayo yakijiri, kumetokea vurugu katikati mwa jiji la Paris zilizohusisha vijana wenye mrengo wa kushoto ambao hawakufurahishwa na ushindi wa Le Pen.
Polisi walipambana nao kwa kuwapiga viboko.Vile vile kumekuwa na maandamano magharibi mwa mji wa Nantes.
Tayari viongozi mbali mbali wa nchi za ulaya wameanza kuonyesha kumuunga mkono Macron.
Msemaji wa Chancellor wa ujerumani Angela Merkel amemtakia kila la heri, na kusifu msimamo wake kuunga mkono Umoja wa Ulaya.
SHARE
No comments:
Post a Comment