Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe,Naibu Waziri
wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole Gabriel na
Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas wakifurahi mara
baada ya kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO
jana mjini Dodoma.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akibonyeza
kitufe kuzindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO jana
mjini Dodoma.Televisheni iyo itaonyesha kazi mbalimbali za
Wizara,Taasisi na Idara za Serikali.Kulia kwake ni Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Mhe.Anastazia Wambura.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe akiangalia
mahojiano yaliyofanyika kati ya Mkurugenzi wa Idara ya Maelezo Hassan
Abbas na Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu kuhusu maadhimisho ya
Muungano yatakayofanyika mjini Dodoma.Mahojiano hayo ni ya kwanza
kupitia televisheni ya mtandaoni ya Idara ya habari-MAELEZO.
Waziri wa
Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Harrison Mwakyembe akizungumza
na menejimenti ya Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo(Hawapo
Pichani) na kuipongeza Idara ya habari kwa kuwa wabunifu.Kulia kwake ni
Naibu Waziri wake Anastazia Wambura,Katibu Mkuu Prof.Elisante Ole
Gabriel na Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari-MAELEZO Dkt.Hassan Abbas.
Picha na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA.
Na Daudi Manongi-MAELEZO.
Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe,Harrison Mwakyembe ameipongeza
Idara ya Habari-MAELEZO kwa ubunifu mkubwa katika kuitangaza Serikali.
ameyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akizindua televisheni ya
mtandaoni ya Idara ya Habari-MAELEZO inayoitwa MAELEZOTV.
“Napenda
nichukue fursa hii kwa kuwapongeza Idara ya Habari kwa kazi nzuri
mnayoifanya katika Wizara hii,nawapongeza kwa ubunifu mkubwa na leo
tunazindua Televisheni ya mtandaoni ya Idara hii kwa mara ya kwanza
katika historia ya Wizara yetu na Idara ya Maelezo kwa ujumla kuwa na”
Alisema Waziri Mwakyembe.
Amesema
kuwa kwa kazi ya kwanza ambayo imeonekana katika televisheni hiyo
imeonyesha weledi wa hali ya juu na kuwataka viongozi wengine wa Wizara
hiyo kuiga mfano mzuri na kuwa wabunifu na kusisitiza kuwa nchi yetu ina
vipaji na ubunifu wa hali ya juu ikiwemo timu yetu ya Vijana ya
Serengeti Boys na n.k
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO,amesema kuanzishwa
kwa televisheni hii ya mtandaoni itasaidia kwa kiasi kikubwa Serikali
katika kutangaza matamko mbalimbali na uzinduzi wake wa mapema utasaidia
kufikisha taarifa mbalimbali kwa jamii husika.
“Sisi
kama Serikali tumekuwa makini katika kuimarisha mawasiliano kati yetu na
wananchi na hii televisheni ya mtandaoni itatusaidia kwa kiasi kikubwa
kufanikisha dhima ya Serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza kazi
zake”,Aliongeza Dkt Abbas.
Mbali na
hayo amesema kuwa kipindi cha kwanza kabisa kuwekwa katika televisheni
hii itakuwa mahojiano ya maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya muungano
waliyofanya na Makamu wa Rais ya Jamhuri ya Muungano Mhe.Samia Hassan
Suluhu.
SHARE
No comments:
Post a Comment