Waziri
wa Elimu na Sayansi Prof. Joyce Ndalichako mapema amewasili katika
Chuo cha Sayansi na Tekinolojia Nelson Mandela Arusha kwa ajili ya
Uzinduzi wa mpango wa African Capacity unaofadhiliwa na Benki ya ADB.
Akizungumza
na wanafunzi wa Chuoni hapo Profesa Ndalichako amesema Atawachukulia
hatua kali waajiri katika sekta ya Elimu watakaowakataza baadhi ya
wafanyakazi waliopata ufadhili wa kwenda masomoni kujiendeleza .
Pia
akiwa kwenye uzinduzi huo waziri alifanikiwa kutembelea maabara
mbalimbali za idara tofauti za Chuo hicho zinazotumika na wanafunzi kwa
ajili ya majaribio na pia alipata wasaaa wakutembelea shamba la migomba
lililopo nje kidogo ya chuo hicho.
Waziri wa Elimu akisalimia na watumishi ya Chuo cha Nelson Mandela leo Asubuhi baada ya kuwasili chuoni hapao .
Pichani
ni wanafunzi wa PHD in material science and Energy lub,Agatha Wagotu na
Joyce Elisadiki wakiwa ndani ya Maabara wakifanya majaribio.
Habari Picha na Imma Msumba
SHARE
No comments:
Post a Comment