ASKARI wa usalama barabarani
wilayani Kibaha mkoani Pwani wakisikiliza elimu juu ya matumizi ya mfumo
wa kubaini stika bandia kwa magari mbalimbali,mfumo ulianzishwa na
mamlaka ya usimamizi wa Bima nchini TIRA. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Jopo la wajumbe kutoka mamlaka
ya usimamizi wa bima nchini wakihakiki stika za bima katika moja ya lori
eneo la mizani Mailmoja Kibaha.(picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima
Tanzania (TIRA),imeanza kampeni endelevu ya kuhakiki magari yenye stika
za bima bandia ili kuondoa wimbi la stika hizo ambalo hulisababishia
serikali kukosa mapato.
Aidha zoezi hilo litawezesha kubaini mtandao wa makampuni yanayotengeneza stika hizo .
Akizindua zoezi hilo mjini
Kibaha, Kamishna wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima nchini, Dk. Baghayo
Saqware ,alisema kampeni hiyo itaendeshwa kwa kusimamiwa na jeshi la
polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani kwa kushirikiana na TIRA.
Alieleza kwamba ,uhakiki huo utafanyika kwa kutumia mfumo wa teknolojia ya TEHAMA-unaoitwa TIRA –MIS .
Saqware alisema,askari wa usalama
barabarani wanapaswa kutumia mtandao na ujumbe wa kawaida kwenda namba
15200 ambapo watapokea maelezo ya halisi ya stika anayoikagua.
Hata hivyo alibainisha
kuwa,wameamua kubuni mfumo huo ili kukomesha wizi unaofanywa na baadhi
ya makampuni yanayotengeneza stika na wamiliki wa magari.
Kamishna huyo alisema,tatizo hilo
linaweza kukua zaidi endapo mamlaka hiyo itaendelea kukaa kimya ikiwa ni
watengeneza wakuu wa stika hizo za bima.
“Tatizo ni kubwa hasa mikoa inayopitiwa na barabara kuu ya Dar es salaam ,Pwani na Arusha”
“Kutokana na hilo tumeona vyema tukaanza kujenga ufa kabla ya ukuta ,Hali isije kuwa mbaya zaidi’alisisitiza Saqware.
Saqware alielezea,wamezindua zoezi
na kampeni hiyo rasmi kwa kuanzia wilaya ya Kibaha kwa kutoa elimu kwa
askari wa usalama barabarani juu ya mfumo huo.
Alisema kila ofisi yao ya kanda itatekeleza zoezi hilo kwa kutoa elimu kwa wananchi,askari wa usalama barabarani na madereva.
Nae kamanda wa usalama barabarani
mkoani Pwani,Abdi Issango ,alisema zoezi hilo limeanzishwa katika muda
muafaka kwani utitiri wa stika feki ni kero kubwa.
Alisema wimbi la stika bandia linakwamisha mapato ya serikali na kuumiza wananchi wasio na hatia.
Kamanda Issango ,itasaidia
kukamata magari yenye stika feki ili kubaini mtandao wa makampuni
mbalimbali yanayotoa bima zisizo halali.
“Kuna kesi nyingi za bima feki ama
wamiliki wengine hutumia stika moja ya bima kwenye magari yake zaidi ya
kumi,kinyume na taratibu za TIRA”alifafanua Issango.
Kamanda Issango ,alisema bima ni
kinga ya ajali ,wahanga wanatakiwa kufidiwa hivyo kama gari limepata
ajali halijakata bima linamnyima mwananchi haki yake ya
matibabu,majeruhi na kifo.
Alisema kwa mkoa wa Pwani hali hairidhishi ,kwani magari mengi
yamekuwa yakifoji ,na kuwa na stika walizozipata kwa njia za mkato.
Kamanda Issango ,alitoa wito kwa
wananchi hasa wamiliki wa mabasi,malori na magari binafsi kuacha kupitia
njia zisizo halali kununua ama kutengeneza stika bandia .
SHARE
No comments:
Post a Comment