Chemba
ya Wafanya biashara, Viwanda na Kilimo ( TCCIA ) imeingia makubaliano
na Chemba ya Biashara ya Uturuki (TOBB) mjini Instanbul.TOBB ni chemba
ya 2 kwa ukubwa duniani ikiwa na wanachama zaudi ya 1,500,000. Ikumbukwe
kuwa Uturuki ni Nchi ya 16 kwa uchumi duniani na kilimo ni Nchi ya 7.
Makubaliano
haya yanafuatia Ziara ya Rais wa Uturuki Nchi Tanzania. Ambapo TCCIA na
TOBB zimekubaliana kushirikiana kwenye kubadilishana ujuzi, uwekezaji
wa pamoja na kukuza biashara .
Pia
TCCIA imefungua ofisi yake ya uwakilishi jijini Instanbul ili kukuza
biashara kati ya Nchi mbili hizi. Ofisi ya diaspora hii utaongozwa kwa
muda na Dr. Miraji.
Zoezi
la kutiliana mkataba na TOBB liliongozwa na Makamu Rais wa TCCIA Bw.
Octa Mshiu akiongozana na Mshauri wa TCCIA Imani Kajula. Kabla ya kwenda
Uturuki ziara hiyo ilianzia nchini Italia.
SHARE
No comments:
Post a Comment