K-VIS
BLOG
BENKI Kuu ya Tanzania imefuta
leseni ya biashara ya Benki ya Kijamii ya Mbinga, Mbinga Community Bank Plc, kuanzia leo Mei 12, 2017.
Taarifa ya Benki Kuu ya Tanzania
iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari leo asubuhi imesema, kufuatia kufutiwa
leseni kwa benki hiyo kuanzia leo Mei 12, 2017 shughuli zote za kibenki nazo
pia zimesitishwa.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania imeiweka
Mbinga Community Bank Plc chini ya
ufilisi na kuiteua Bodi ya Bima ya Amana kama mfilisi kuanzia leo Mei 12, 2017
Uamuzi huu umechukuliwa baada ya
Benki Kuu ya Tanzania kujiridhisha kuwa Mbinga
Community Bank Plc ina upungufu mkubwa wa mtaji na ukwasi kinyume na
matakwa ya Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya wmaka 2006 na kanuni zake.
“Upungufu huu wa mtaji na ukwasi
unahatarisha usalama wa sekta ya fedha, na kwamba kuendelea kwake kutoa huduma
za kibenki kunahatarisha usalama wa amana za wateja,” taarifa hiyo imeeleza.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
imeuhakikishia umma kuwa “itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika
mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.”
Benki Kuu ya Tanzania imechukua
uamuzi wa kuifunga benki hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 56(1) (g), 56(2) (a),
(b) na (d), 58(2) (i), 11(3) (j), 61(1) na 41(a) cha Sheria ya Mabenki na
Taasisi za Fedha ya mwaka 2006.
Aidha, Benki Kuu ya Tanzania
imewataka wenye amana, wadai na wadaiwa wa iliyokuwa Mbinga Community Bank Plc
kuwa wavumilivu wakati Mfilisi atakapokamilisha taratibu na kwa wakati muafaka
atawafahamisha wenye amana, wadai na wadaiwa utaratibu wa malipo ya madai,
ulipaji wa madeni na taratibu nyingine zitakazohitajika kwa mujibu wa sheria.
Hatuahiyo ya BoT, imekuja siku
nne tu tanguichukue hatua kama hiyo, kwa kuifutia leseni benki ya FBME kwa
sababu kama hizo.
SHARE
No comments:
Post a Comment