TRA

TRA

Friday, May 12, 2017

Rais Moon wa Korea Kusini afutilia vitabu vya historia shuleni vilivyotolewa na serikali

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, leo amefutilia mbali vitabu vya kusoma vya historia kwa wanafunzi, ambavyo vilianzishwa na mtangulizi wake, Park Guen-Hye.

Moon amesema vitabu hivyo vilikuwa na mawazo yaliyopitwa na wakati na kibaguzi yaliyoegemea upande mmoja na yanayolenga kuwagawanya wananchi. Utawala wa mtangulizi wake, Park Geun-Hye, ulianzisha vitabu hivyo ambavyo viliandikwa na serikali kutumiwa na wanafunzi wa shule za kati na sekondari.

Lakini Moon amesema baadhi ya mawazo katika vitabu hivyo yaliegemea sera za siasa za mrengo wa kushoto na kupendelea sera za Korea ya Kaskazini. 

Serikali ya Park ilivichapisha vitabu hivyo mwaka huu licha ya pingamizi kutoka kwa wakosoaji wa kiliberali waliotizama hatua hiyo kama njama ya kusifia uongozi wa kidikteta wa zamani marehemu Park Chung-Hee, baba mzazi wa Park Guen-Hye, aliyeondolewa madarakani kwa tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger