Katibu
Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akizungumza na
wataalamu wa kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia
(Costech), Jukwaa la Bioteknojia na Uhandisi Jeni (OFAB) pamoja na
wanahabari walipofika ofisini kwake wakiwa katika ziara ya kutoa mafunzo
ya kilimo chenye tija kwa maofisa ugani wa mkoa huo leo.
Mtaalamu
wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru
jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akitoa maelezo kwa Katibu Tawala wa
Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba kabla ya kuanza ziara ya mafunzo
hayo.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akiwaonesha shamba la
mfano la mahindi ambalo lipo nje ya ofisi yake wataalamu hao wa kilimo
pamoja na wanahabari (hawapo pichani). Kulia ni Mshauri wa Jukwaa la
Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange na kushoto ni Mratibu
wa Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Geita (RAS), Selestine Gesimba akionesha shamba la
mfano la alizeti ambalo lipo nje ya ofisi yake. Kushoto ni Mratibu wa
Jukwaa hilo Tanzania, Philbert Nyinondi.
Zao la alizeti likioneshwa.
Ofisa
Program wa OFAB kutoka Shirika la AATF, Suleiman Okoth (wa nne kutoka
kulia), akiwa na wataalamu hao wakilimo wakati wakiangalia bwawa la
samaki la mfano lililopo nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.
Ofisa
Uvuvi wa Mkoa wa Geita, Tito Mlelwa akiwa mbele ya bwala la samaki la
mfano lililopo nje ya ofisi ya mkuu wa mkoa huo huo wakati akizungumza
na wanahabari.
Jengo la Ofisi la Halmshauri ya Wilaya ya Chato linavyoonekana.
Maofisa Ugani wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato wakiwa kwenye mafunzo ya kilimo chenye tija.
Ofisa Ugani kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, David Makabila (kulia) akizungumza kabla ya kuanza kwa mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wakifuatilia mada katika mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wakiandika wakati wa mafunzo hayo.
Mafunzo yakiendelea.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Chato, Martin Ndilanha (kulia), akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mafunzo
yakiendelea. Kutoka kulia ni Ofisa Program wa OFAB kutoka Shirika la
AATF, Suleiman Okoth, Ofisa Ugani wa Wilaya ya Chato, Charles Ntaki na
Mratibu wa OFAB Tanzania, Philbert Nyinondi.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Chato, Elias Makory akifungua mafunzo hayo.
Mshauri
wa Jukwaa la Kilimo na Bioteknojia (OFAB), Dk.Nicholaus Nyange (kulia),
akitoa mada katika mafunzo ya kilimo ya siku moja kwa maofisa ugani wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita leo ambayo yameratibiwa na
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), kupitia Jukwaa hilo.
Mtaalamu
wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiliguru
jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon akitoa mada katika mafunzo hayo.
Na Dotto Mwaibale, Chato
MAOFISA
Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita wameombwa kuwa
weredi zaidi katika masuala ya kilimo ili elimu waliyonayo waweze kuitoa
kwa wakulima ili nao waweze kulima kilimo chenye tija cha zao la mihogo
ili zao hilo liweze kukubalika katika soko la kimataifa.
Mwito
huo umetolewa na Mtaalamu wa masuala ya mizizi kutoka Kituo cha Utafiti
wa Kilimo cha Ukiliguru jijini Mwanza, Dk. Jeremiah Simon wakati akitoa
mafunzo kwa maofisa Ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani
Geita leo ambayo yameandaliwa na Tume ya Sayansi ya Teknolojia (Costech)
kupitia Jukwaa la Wazi la Bioteknolojia kwa manufaa ya kilimo (OFAB).
Alisema
hivi sasa nchi ya China na Tanzania zimesaini mkataba wa ununuzi wa zao
la muhogo jambo ambalo ni fursa kwa wakulima wetu wa hapa nchini
wakiwemo wa kutoka wilaya ya Chato.
"Hii
ni fursa kubwa kiuchumi lakini ni vema sasa tukaingia katika kilimo
chenye tija ili mihogo yetu iweze kuingia katika soko la kimataifa
badala ya kuendelea na kilimo kisicho na tija" alisema Simon.
Katika
kuonyesha kuwa swala la kilimo na shuguli za ugani ni muhimu katika
kusaidia kuboresha kilimo na kuongeza tija kwa wakulima katibu tawala wa
mkoa wa Geita, Selestine Gesimba ameanzisha mashamba darasa ya mfano ya
mazao mbalimbali nje ya ofisi yake.
Amesema
lengo la kufanya hivyo nje ya ofisi yake ni kuonyesha kwa vitendo dhana
nzima ya ugani kwani anaamini mkulima anaamini akiona kwa macho yake
kuliko kusikia.
Hata
hivyo amesema kila halmashauri itatakiwa kuwa na mashamba madogo ya
mfano kwenye ofisi zao kuonyesha kilimo bora cha mazao muhimu kwenye
wilaya pamoja na ufugaji bora wa mifugo na samaki.
Katibu
tawala huyo wa mkoa wa Geita amesema kwa kufanya hivyo kuanzia mkoani
wilayani na kwenye kata na vijiji kwa kusimamiwa na wataalamu wa mazao
na mifugo wakulima watajifunza na tija itaonekana.
Nje
ya ofisi hiyo ya katibu tawala wa mkoa na mkuu wa mkoa wa Geita
wameweka vishamba vidogo vya mahindi, Alizeti, Maharage pamoja na bwawa
la kufugia samaki ambalo wananchi watakwenda kujifunza lakini
wanajiandaa kuweka na mifugo mingine kama ng'ombe,kuku na mifugo
mingine.
Akiwasilisha
mada yake juu ya kilimo bora cha zao la pamba mtafiti na mtaalamu wa
magonjwa ya mazao kutoka kituo cha utafiti wa kilimo Ukiliguru Stellah
Chirimi amewataka maafisa Ugani hao kushauri wakulima kila mtu kuwa na
ekari moja ya Pamba iliyolimwa na kuhudumiwa kisasa ili kupata tija.
Amesema
wakulima wengi hawazingatii kilimo bora cha kupanda kwa mstari ili kuwa
na idadi inayotakiwa ya miche kwenye shamba na kujikuta wanalima ekari
nyingi ambazo hazina matunzo kabisa hali ambayo inawapekea kupata mavuno
yasiyo na tija.
Amesisitiza
umuhimu wa kila Ofisa Ugani kuwa na mashamba madogo ya mfano kwenye
kata zao ambayo wakulima watakwenda kuona na kujifuza kuliko kutumia
mashamba ya wakulima pekee.
SHARE
No comments:
Post a Comment