Aliyekuwa mgombea
wa urais nchini Marekani Hillary Clinton amewalaumu wadukuzi wa Urusi na
mkurugenzi wa Ujasusi nchini humo kwa kushindwa kwake katika uchaguzi
mkuu uliopita.
Aliambia mkutano mjini New York kwamba angeshinda kura hiyo iwapo uchaguzi huo ungefanyika tarehe 20 mwezi Oktoba kabla ya kuchapishwa kwa barua ya mkurugenzi wa FBI James Comey akilielezea bunge la seneti kwamba FBI imeanzisha uchunguzi kuhusu hatua yake ya kutumia barua pepe za binafsi.
Alisema kwamba alikuwa amefanya kampeni nzuri na akapoteza kutoka na maswala yaliofanyika katika kipindi cha siku kumi za mwisho.
Anasema kuwa sasa amerudia uanaharakati akisema hatua yake inalenga kuweka upinzani mkali dhidi ya rais Trump ambaye amemkosoa kwa sera zake za kigeni mbali na utumizi wake wa mtandao wa Twitter.
SHARE
No comments:
Post a Comment