Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa
Dkt Jesca Msambatavangu akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi
mfawidhi wa mkoa wa Iringa kusomewa shitaka lake la jinai namba 65
la mwaka 2017 aliloshitakiwa kwa kumpiga Neema Nyongole mkazi wa
Kibwabwa mjini Iringa ,mahakama hiyo imemwachia kwa dhamana hadi
tarehe 1/6/2017 kesi hiyo itakapo tajwe tena mahakamani hapo baada
ya upelelezi wake kuendelea (picha na Francis Godwin matukiodaimaBlog )
Na MatukiodaimaBlog
MAHAKAMA ya hakimu mfawidhi mkoa wa Iringa imemwachia kwa
dhamana aliyekuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Dkt Jesca
Msambatavangu (41)aliyeshitakiwa kwa kesi yake ya jinai namba 65 ya
mwaka 2017.
Akisoma shitaka hilo jana
mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Iringa jana mwanasheria upande
wa jamhuri Alex Mwita alisema kuwa Msambatavangu anadaiwa
kumshambulia Neema Nyongole mkazi wa Kibwabwa katika Manispaa ya
Iringa Februari 17 mwaka huu katika eneo la Kibwabwa kosa hilo
ambalo ni kinyume na kifungu cha seria kanuni ya adhabu sura namba
16 marejeo mwaka 2002.
Alisema upalelezi wa
kesi hiyo unaendelea na kutokana na kosa hilo upande wa jamhuri
hauna pingamizi ya dhamana kwa mtuhumiwa huyo .
Dkt
Msambatavangu alikana kuhusika na kosa hilo huku hakimu
anayesikiliza kesi hiyo David Ngunyale alisema kuwa dhamana kwa
mshitakiwa ipo wazi na kumtaka kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa
na wadhamini wawili waamini ambao kila mmoja atasaini dhamana ya
shilingi milioni 1 .
Idadi ya wadhamini
waliofika mahakamani hapo waliweza kutimiza masharti hayo na hivyo
kufanikiwa kutoka kwa dhamana hadi kesi hiyo itakakapo tajwa tena
mahakamani hapo June 1 mwaka huu .
Dkt
Msambatavangu anayetetewa na mawakili wawili Alfred Mwakingwe na
Jackson Chaula alifikishwa mahakamani hapo majira ya saa 4;8 asubuhi
kwa gari la polisi
Toyota Land Cruiser
akiwa amekaa siti ya mbele huku nyuma kukiwa na ulinzi mkali wa
askari wa kikosi cha FFU na kuingizwa mahabusu ya mahakama kwa
muda kabla ya kufikishwa mahakamani .
Idadi
kubwa ya wananchi walifika katika mahakama hiyo kusikiliza kesi
hiyo wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na maendeleo
(Chadema) wakiongozwa na mwenyekiti wake wa wilaya Frank Nyalusi ,
Mstahiki meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe ,naibu meya wake na
watu mbali mbali huku zaidi ya watu sita walikuwa na barua za dhamana
na muda wote akiwa mhakamani hapo Dkt Msambatavangu alikuwa mwenye
sura ya furaha .
|
No comments:
Post a Comment