Taarifa kwa
vyombo vya habari
Kampuni ya Coca-Cola leo imezindua katika soko la Tanzania soda mpya ya Coca-Cola Bila Sukari.
Uzinduzi wa soda hii mpya umefanyika katika kiwanda
cha Bonite mkoani Kilimanjaro ambapo pia baadaye utafanyika katika mikoa ya
Mwanza,Dar es Salaam na Mbeya.
Soda mpya ya
‘Coca-Cola Bila Sukari ladha yake imeboreshwa zaidi kutokana na soda isiyo na sukari iliyokuwa inatengenezwa hapo
awali ya Coca-Cola Zero ambapo soda mpya
ladha yake inashabihiana na soda ya Coca-Cola asilia lakini haina sukari
kabisa.
Tangia mwaka 2006
wakati soda ya Coke Zero imeingia kwenye masoko, kampuni ya Coca-Cola imekuwa
ikifanya jitihada kuhakikisha inatengeneza soda mpya ya Coca-Cola isiyo na
sukari lakini yenye ladha sambamba na Coca-Cola asilia na imefanikiwa kuja na
soda mpya ya ‘Coca-Cola Bila Sukari ‘
kinywaji ambacho kitawezesha watumiaji wa Coca Cola kuipata kwa ladha
asilia hata kama watachagua kuipata
isiyotengenezwa kwa sukari.
"Soda ya ‘Coca Cola Zero’ ina ladha nzuri
pia,lakini pamoja na ubora wake timu ya Coca-Cola imekuwa ikifanyia kazi
kuhakikisha inapatikana soda isiyo na
sukari lakini yenye ladha inayoshabiana na Coca-Cola asilia . Ubunifu wa
wataalamu wetu umewezesha kupatikana soda mpya ya ‘Coca Cola Bila Sukari’ ambayo inatoa wigo
kwa wateja kuwa na chaguo la kupata kinywaji cha Coca-Cola kwa radha asilia
kwa kadri wanavyotaka,ikiwa na ladha ya
sukari ama isiyo na sukari," alisema Mkurugenzi wa Mauzo na Masoko wa Bonite bottlers,Christopher
Loiruk
Aliongeza kuwa
lengo kubwa ni kuhakikisha watumiaji wa soda ya Coca-Cola wanafurahia ladha yake
halisi na asilia wanapokunywa soda yenye sukari au Coca-Cola Bila Sukari.
Soda mpya ya
Coca-Cola Bila Sukari itakuwa kwenye
mwonekano mpya ambapo vifungashio vyake vya chupa na kopo vinafanana na
vifungashio vya Coca-Cola asilia na
maandishi yake yametenganishwa na
mstari wenye rangi nyekundu.
Soda za Coca Cola
Bila Sukari zitakuwa kwenye soko la
Tanzania kuanzia mwezi huu katika sehemu
zote zinapouzwa soda na bei yake ni sawa na
soda aina nyingine zote zinazotengenezwa na kusambazwa na kampuni ya
Coca-Cola.
SHARE
No comments:
Post a Comment