Francesco Totti alitokwa na machozi alipokuwa anaaga baada ya kucheza mechi yake ya mwisho katika klabu ya AS Roma.
Mshambuliaji huyo wa umri wa miaka 40 amechezea klabu hiyo kwa miaka 25.Katika kipindi hicho, amefunga mabao 307 katika mechi 786 alizocheza.
Aliingia uwanjani mara ya mwisho dakika ya 54 mechi yao dhidi ya Genoa.
Roma walishinda 3-2 kupitia bao la dakika ya mwisho la Diego Perotti ambalo liliwahakikishia nafasi ya kucheza hatua ya makundi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Baada ya mechi, Totti alisoma barua kwa mashabiki, na kusema: "Naogopa. Sijui siku za usoni zitakuwaje."
"Tafakari, kwamba wewe ni mtoto na umo katikati ya ndoto nzuri...na mamako anakuamsha uende shuleni.
"Unajaribu kurejea kwenye ndoto yako...unajaribu sana lakini huwezi.
"Wakati huu si kwamba ni ndoto, ni uhalisia. Na siwezi kurejea tena."Nahodha Totti pia alipewa nambari 10 iliyowekwa kwenye fremu, nambari ya jezi yake.
Mkewe na watoto pia walikuwa uwanjani.
Anatarajiwa kuwa mkurugenzi katika klabu ya Roma lakini kumekuwepo na taarifa kwamba huenda akaelekea kwingine.
CHANZO: BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment