Na Jumia Travel Tanzania
Ni
jambo la kawaida kuachwa na usafiri kama vile basi, boti, treni au
ndege licha ya kufanya maandalizi ya kutosha. Baadhi ya sababu
zinazoweza kuchangia mtu mpaka kuachwa na usafiri ni kama vile foleni
barabarani, ajali au usafiri kupata matatizo na kukosea muda wa
kuwasili.
Hali
ya kuachwa na usafiri ni ngumu sana kama haijawahi kukutokea kabla na
hauna mbinu mbadala ya kukuwezesha kusafiri kama ulivyokukusudia. Zipo
hatua kadhaa za kufuata pindi uchelewapo ndege ambazo Jumia Travel
ingependa uzifahamu na kuzizingatia pindi utakapokumbwa na changamoto
kama hii.
Wasiliana
na shirika la ndege unalosafiri mara moja. Kitu cha kwanza kabisa baada
ya kugundua kwamba utachelewa au umechelewa ndege ambayo ulitakiwa
kusafiri nayo ni kuwasiliana na shirika husika. Mara nyingi mawasiliano
huwemo kwenye tiketi au tovuti ya shirika. Kwa kufanya hivyo utajua ni
msaada gani wanaweza kukupatia kulingana na hali uliyopo.
Kuwa
makini na sheria na masharti ya tiketi uliyokata. Kila shirika la ndege
linakuwa na taratibu za uendeshaji wa safari zake. Zipo ambazo
zinawasafirisha na ndege nyingine wateja wao waliochelewa, zingine siku
inayofuata kama hamna kwa siku hiyo na zingine kutoza malipo ya ziada
kwa kuchelewa ndege. Kwa hiyo kabla ya kukata tiketi ulizia taarifa hizo
au soma kwenye tiketi yako kama zipo.
Usihamaki/usiwe
na hofu. Wewe sio wa kwanza kuachwa na ndege hali hiyo ishawakuta watu
wengi hivyo vuta pumzi na tuliza akili yako ili ujue nini cha kufanya.
Usipohamaki utaweza kupata suluhu ya tatizo haraka sana kama vile
kuulizia cha kufanya, kuahirisha au kutafuta uwanja wa ndege ulio karibu
ili usafiri na kuwahi shughuli zako kama ulivyopanga. Kwani kama
kuchelewa umekwisha chelewa hakuna cha kufanya kutokana na hali hiyo.
Ulizia
kwa wafanyakazi wa kampuni husika ya ndege machaguo uliyonayo. Kama
umeshindwa kupata mawasiliano au haujui taratibu za shirika la ndege
ulilokatia tiketi ya kusafiri basi ni vema ukauliza. Mashirika mengi
yanakuwa na ofisi kwenye viwanja vya ndege au kama hawana basi ulizia
wafanyakazi wa pale naamini wao wana uzoefu mkubwa wanaoweza kukupatia.
Lipia
gharama za ziada baada ya kukosa ndege kama ulishafika tayari. Kama
unaona kwamba utachelewa shughuli zako huko uendako basi huna budi
kuongeza pesa kidogo ili uweze kusafiri na ndege inayofuata. Hii itakuwa
nafuu zaidi kuliko kukata tiketi upya au kuahirisha safari. Kwa hiyo ni
vema pia kuwa na fedha au chanzo za ziada pindi unapokuwa unasafiri
kwani chochote kinaweza kutokea.
Tazama
kama kuna ndege zingine zinazoelekea mahali uendapo. Kwa kawaida kwenye
viwanja vya ndege vingi kunakuwa na ubao unaoonyesha ndege za mashirika
tofauti zinazokwenda sehemu mbalimbali kwa siku hiyo. Hivyo inaweza
kuwa fursa kwako kwa kufanya maamuzi ya kukata tiketi ili kuwahi
shughuli zako.
Tumia
muda huo kufanya mambo mengine. Kuchelewa safari haimaanisha kwamba
ndiyo mwisho wa maisha. Kwa mfano upo Arusha na umechelewa ndege ya
kukurudisha Dar es Salaam kwa siku hiyo, unaweza kuamua kutembelea
vivutio kadhaa vilivyopo karibu na eneo hilo kama vile hifadhi ya
Serengeti au Ngorongoro au hata Mlima Kilimanjaro.
Ifahamishe
hoteli utakayofikia mapema. Mara nyingine huwa tunafikia kwenye hoteli
kwa mahali tunapoelekea labda uwe unarudi nyumbani. Kwa hiyo nina
uhakika utakuwa umelipia hoteli wakuhifadhie chumba au kuomba usafiri wa
kuja kukuchukua uwanja wa ndege. Ifahamishe hoteli utakayofikia mapema
kwamba utachelewa au utafika siku inayuofuata ili kuondoa usumbufu kwao
na kulipishwa gharama za ziada.
Jifunze
kutokana na makosa yako. Kufanya makosa ni sehemu ya kujifunza mambo
mengi maisha yetu. Hivyo basi hakikisha kwamba baada ya kuchelewa safari
hii utakuwa makini zaidi wakati mwingine. Kama ulichelewa kwa sababu ya
usafiri basi hakikisha unatoka mapema zaidi, kama ni ulikosea kuangalia
muda basi muombe mtu wa karibu yako akukumbushe.
Sababu
ni nyingi ni zingine haziwezei kuzuilika kwa upande wa abiria na hata
kwa shirika la ndege. Kuna wakati mwingine unaweza kuchelewa ndege
kutokana na sababu za kiufundi za shirika lenyewe. Mara nyingi kwa
sababu kama hizo abiria huwa wanafidiwa na mashirika ya ndege. Lakini
kama ni sababu zako binafsi, Jumia Travel inakuasa kwamba uwe makini
kwani utaishia kupoteza muda, kuvuruga mipango yako na kuingia gharama
za ziada usizozitarajia.
SHARE
No comments:
Post a Comment