Na Francis Dande
Mradi
wa Ujenzi wa Barabara inayounganisha Daraja la Nyerere na barabara
inayotoka Kigamboni hadi Kibada unaotekelezwa kwa ubia kati ya Serikali
na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), mradi huu wa ujenzi wa
barabara yenye urefu wa kilometa 1.2 unatarajia kukamilika ndani ya
kipindi cha miezi sita.
Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,Prof.
Godius Kahyarara, amesema kuwa barabara hiyo itakuwa na njia sita
pamoja na mzunguko (Round Abaout) wenye vipande vya barabara za mita 500
kwa kila kimoja, barabara hii itakuwa na uwezo wa kupitisha yenye uzito
wa tani 55.
'Aliongeza kuwa ili kutekeleza mradi huuNSSF tayari imetenga Shilingi bilioni 21 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu'.
Aidha
alisema kuwa kukamilika kwa mradi huu kutasaidia wakazi wa Kigamboni
kutumia barabara hii muda wote wa mwaka bila kuathiri mabadiliko ya hali
ya hewa. Pia kutasaidia ukuaji wa viwanda kwa kusaidia usafirishaji wa
bidhaa na malighafi.
Barabara
hiyo inajengwa na mkandarasi anayejenga barabara hii ndiye aliyejenga
mradi mkubwa daraja la Nyerere na ameanza kazi toka Mei 26 mwaka huu na
anatarajiwa kukamilisha ujenzi huo Novemba 25 mwaka.
Naye
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour alisema
kuwa kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizo za kuunganganisha na daraja
la Nyerere na barabara ya Kigamboni-Kibada Kigamboni kutatoa fursa kwa
wakazi wa eneo la Kigamboni kuwa na usafiri wa uhakika kwa wakati wote.
Jiwe la Msingi la mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada lililowekwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour. (Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Mkurugenzi
Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi
wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya
Kigamboni-Kibada yenye urefu wa kilometa 1.2 wakati kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour alipoweka jiwe la Msingi.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour, akizindua wa jiwe la Msingi la Ujenzi wa mradi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Meneja
Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal Mruma (kushoto),
akibadilishana mawazo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour
Hamad Amour (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Kiongozi
wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (wa pili kulia)
akiwa ameongozana na Meneja Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal
Mruma (kulia), wakati wa uzindua wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Meneja
Mradi wa Daraja la Kigamboni, Mhandisi Jamal Mruma (kushoto),
akibadilishana mawazo Kiongozi wa Mbiuo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,
Amour Hamad Amour (katikati) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara wakati wa uwekaji wa jiwe la Msingi la Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiungo kati ya Daraja la Nyerere na Barabara ya Kigamboni-Kibada.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara, akisalimiana na mmoja wa wakimbiza Mwenge wa Uhuru, Bahati Mwinuguta.
Baadhi ya viongozi wa dini na taasisi wakiwa katika hafla hiyo.
Maofisa wa NSSF wakiwa katika picha ya pamoja.
Baadhi ya Menejimenti ya NSSF wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa NSSF.
Kiongozi
wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour (katikati) akiwa
katoka picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara (kushoto kwake) baada ya kuweka jiwe la Msingi.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyarara (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba wakati wa uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Daraja la Nyerere na barabara inayotoka Kigamboni hadi Kibada.
SHARE
No comments:
Post a Comment