Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov akikabidhiana hati ya
makubaliano ya mkataba na Rais wa Klabu ya Simba Evance Aveva ukiwa ni
mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya Bilion
4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa
Mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya SportPesa Pavel Slavkov pamoja na Rais wa Klabu
ya Simba Evance Aveva wakisaini hati ya makubaliano ya mkataba na ukiwa
ni mkataba wa udhamini wa kipindi cha miaka mitano wenye thamani ya
Bilion 4.9 uliofanyika leo katika ukumbi wa Uwanja wa Taifa. Kulia ni
Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania Abbas Tarimba.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Kampuni ya SportPesa imeingia mkataba wa miaka mitano wa kuidhamini klabu ya Simba ukiwa na thamani ya Bilion 4.9 .
Kampuni
hiyo inayojishughulisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu nchini
Kenya imeweza kuingia nchini Tanzania na kuja kufanya uwekezaji kwa
klabu mbalimbali za mpira wa miguu.
Utiaji
saini wa makubaliano ya mkataba huo umefanyika jioni hii katika ukumbi
wa Uwanja wa Taifa na kushuhudiwa na wadau mbalimbali wa mpira nchini.
Rais
wa Klabu ya Simba Evance Aveva amesema mkataba huu utaweza kuwasaidia
katika kuendelea kutoa hamasa kwa timu yao kufanya vizuri zaidi.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa SportPesa nchini Abbas Tarimba amesema kuwa
wamefurahi sana kuingia mkataba na Timu ya Simba na mkataba wao utakuwa
katika hatua tofauti kulingana na makubaliano waliyoyaingia.
Amesema
kwa mwaka wa kwanza Klabu ya Simba watapata milioni 880 na katika miaka
mitatu inayofuata watapata nyongeza ya asilimia 6 huku mwaka wa mwisho
wa mkataba huo klabu hiyo itafaidika kwa kupata bilioni 1.08.
Mbali
na hilo Tarimba amesema kuwa klabu ya Simba itafaidika kwa kupata fedha
mbalimbali kama hamasa iwapo wataweza kupata ubingwa kwa kupewa bonus
ya milioni 100 au kushiriki michuano ya kimataifa.
Kabla
ya utiaji saini wa mkataba huo Simba iliweza kutoka na ushindi wa goli
2-1 dhidi ya stand United magoli yakifungwa na Laudit Mavugo na Juma
Luizio huku la Stand likifungwa na Kasim Selembe.
SHARE
No comments:
Post a Comment