Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imesema kuwa Serikali ya India
imeahidi kutoa dola milioni 500 kwa ajili utekelezaji wa miradi ya maji
katika miji 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar katika awamu ya tatu katika
mwaka wa fedha 2017/18.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe.Eng.Isack Kamwelwe
akijibu Swali la Mbunge wa Tumbatu Mhe.Juma Othman Hija leo Bungeni
Mjini Dodoma.
“Katika
bajeti ya mwaka 2016/17 Wizara yangu ilitoa taarifa ya mchango mkubwa
inaoupata kutoka Serikali ya India ili kuboresha huduma ya Maji nchini
kupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Serikali hiyoa”,Aliongeza
Mhe.Kamwelwe.
Aidha
katika awamu ya tatu hatua inayoendelea kwa sasa ni kufanya manunuzi ya
Mhandisi Mshauri atayefanya mapitio ya usanifu wa miradi na uandaaji wa
makabrasha ya zabuni kwa ajili ya ujenzi ambapo kazi ya ujenzi
zinatarajiwa kuanza katika mwaka wa fedha 2017/18.
Amesema
kuwa katika awamu ya kwanza Serikali ilipata dola za kimarekani Milioni
178.125 ambapo kazi zilizotekelezwa katika awamu hiyo ni upanuzi wa
mradi mkubwa wa Ruvu Juu,Ujenzi wa bomba kuu kutoka Mlandizi hadi
Kimara,Pia Ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji katika Jiji la Dar es
Salaam pamoja na ujenzi wa mradi Chalinze.
Katika
awamu ya Pili Serikali ya India itatoa dola milioni 268.35 kwa ajili ya
mradi mkubwa wa kutoa maji katika mradi wa KASHWASA kutoka kijiji cha
Solwa kwenda katika miji ya Tabora,Igunga,Nzega,Tinde na Uyui pamoja na
Vijiji 89 vinavyopitiwa na bomba kuu umbali wa kilomita 12 kila upande
uku wakandarasi wa kutekeleza mradi huo wamepatikana na wapo katika
hatua za utekelezaji.
SHARE
No comments:
Post a Comment