TRA

TRA

Wednesday, May 17, 2017

Kikwete kuhudumu katika baraza la wakimbizi duniani

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


Aliyekuwa Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ameteuliwa kuhudumu katika baraza kuu la wakimbizi duniani WRC, ambalo ni kundi huru la viongozi na wavumbuzi wanaolenga kubuni mbinu mpya za kutatua mizozo ya wakimbizi.

Kulingana na gazeti la The Citizen nchini Tanzania, taarifa kwa vyombo vya habari ilimtaja Kikwete kuwa mwenyekiti mwenza wa baraza hilo lililopo chini ya uenyekiti wa waziri wa masuala ya kigeni nchini Canada Lloyd Axworthy.
Gazeti hilo limesema kuwa Hina Jinali kutoka Pakistan na Rita Sussmith kutoka Ujerumani watafanya kazi pamoja na  Kikwete kama wenyekiti wenza huku Paul Heinbecker akichaguliwa kama naibu huku naye Fen Hamson akihudumu kama mkurugenzi.

           Rais mstaafu Jakaya Kikwete
Taarifa hiyo imesema kuwa miongoni mwa mengine, baraza hilo litatoa ushauri wa marekebisho na uvumbuzi ili kuimarisha mfumo wote wa wakimbizi duniani.
Baraza hilo litaleta mabadiliko ili kusaidia kuhakikisha kuwa ushirikiano wa kimataifa kwa wakimbizi unaeleweka, unafanyika kwa njia ya usawa na haki, ilisema taarifa hiyo.
Baraza hilo pia litashirikisha madiwani 17 wa mabaraza.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger