Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Issa
Gavu akisoma hotuba ya kufunga semina kuhusu elimu ya Mtangamano wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake. Semina hiyo iliandaliwa na
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifanyika
Pemba kuanzia tarehe 15 - 18 Mei 2017. Wengine katika picha, kushoto ni
katibu wa Wizara hiyo, Bw. Salum Salum na Mkurugenzi kutoka Wizara ya
Mambo ya Nje, Bw. Eliabi Chodota.
Kulia ni Mbunge wa Wete, Mhe. Ali Mbarouk akifuatilia kwa makini semina ya mtangamano.
Washiriki wa semina hiyo ambao wengi wao walikuwa wajasiriamali wakisikiliza hotuba ya kufunga semina.
Washiriki wengine wakifuatilia hotuba ya Mhe. waziri wa Nchi.
Mhe. Waziri wa Nchi akiendelea kuwahutubia wana semina na watu wengine waliohudhuria sherehe za ufungaji.
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Gavu na washiriki wa semina.
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Nje, Bi. Mindi Kasiga akiwasilisha mada kuhusu Diplomasia ya Umma kwa
wana semina hiyo.
Wajumbe wa semina wakisikiliza mada kuhusu Diplomasia ya Umma.
Bi. Mindi akiendelea kuwasilisha mada.
Prof. Ammon Mbelle kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam akiwasilisha mada kuhusu Sera ya Mambo ya Nje kwenye semina hiyo.
Mchumi
kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Elly Chuma akiwasilisha mada kuhusu
utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika Diplomasia
yaUchumi.
Wajumbe wa Semina wakifuatilia mada.
Mjumbe wa Semina akichangia mada.
Watoa mada wakipongezwa na wajumbe wa semina.
Serikali
ya Zanzibar imeahidi kuwa itaendelea na jitihada za kuimarisha huduma za
kiuchumi kwa madhumuni ya kuweka mazingira mazuri ya kibiashara ili
wananchi waweze kunufaika na fursa zinazopatikana kwenye Mtangamano wa
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Mhe. Issa Gavu alipokuwa anafunga semina ya siku nne kuhusu
mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na fursa zake iliyofanyika
Pemba kuanzia tarehe 15 hadi 18 Mei 2017.
Mhe. Gavu
alitoa wito kwa wanasemina hao ambao wengi wao walikuwa ni
wajasiriamali kutengeneza bidhaa zenye ubora kwa kuzingatia mabadiliko
ya teknolojia ya ulimwengu wa sasa ili ziwe na uwezo wa kushindana na
bidhaa nyingine katika soko la EAC.
Aidha,
Mhe. Gavu aliahidi kuwa Serikali itasaidia wajasiriamali washiriki
makongamano, semina, maonesho na warsha mbalimbaili zinazofanyika nchini
na nje ya nchi ili iwe fursa kwao kujifunza mambo mapya yanayoendana na
ulimwengu wa sasa kwa lengo la kuboresha biashara zao.
Mhe. Gavu
aliwasihi wote waliopata na watakaopata fursa za mafunzo kuwa mabalozi
wazuri kwa wenzao ili kwa pamoja watumie mbinu, ujuzi na uzoefu
wanaoupata kukabili changamoto za ushindani wa soko kulingana na
mahitaji ya sasa.
Alisisitiza
umuhimu wa nchi zote wanachama wa EAC kuwahudumia raia wa nchi zote kwa
usawa bila ubaguzi. Alisema endapo nchi moja ikiwa na tabia ya
kunyanyasa raia wa nchi nyingine inaweza kusababisha dhana ya kulipiza
kisasi hatimaye vurugu na kuleta mkanganyiko katika Jumuiya.
Vile
vile, Waziri wa Nchi alitoa wito kwa nchi zote wanachama kushirikiana
kwa pamoja kudhibiti biashara ya magendo. "Sio sahihi kwa nchi moja
kufumbia macho biashara ya magendo kwa kutochukua hatua dhidi ya
wanaoingiza na kununua bidhaa za magendo". Mhe Gavu alisema. Zanzibar
inakabiliwa na biashara ya magendo ya zao la karafuu ambayo
inasafirishwa kwa njia za panya kwenda nchi za jirani.
Kwa
upande wao wajasiriamali wameahidi kuwa watatumia mafunzo waliyopata
kulikabili Soko la EAC bila khofu yeyote kama ilivyokuwa hapo awali.
Semina
hiyo ya siku nne ilifunguliwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga na ilitolewa na wataalamu wa
Wizara kwa kushirikiana na Prof. Ammon Mbelle kutoka Chuo Kikuu cha Dar
Es Salaam.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 18 Mei, 2017
SHARE
No comments:
Post a Comment