TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI –PRESS RELEASE
WATUMIAJI WA HUDUMA ZA TRENI ZA ABIRIA
WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
Watumiaji
wa huduma za usafiri wa treni za abiria za Kampuni ya Reli Tanzania
(TRL) wametakiwa kuzingatia sheria za matumizi ya usafiri huo ili
kuepuka adhabu ya kufungwa jela miezi sita.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka uongozi wa TRL umeainisha kuwa matumizi ya
usafri wa abiria unasimamiwa na sheria , kanuni ,taratibu na masharti
maalum. Mojawapo limetajwa ni kutodandia mabehewa baada ya milango
kufungwa.
Uongozi
katika taarifa hiyo umesisitiza kuwa endapo mtu atafanya kosa hilo
atafikishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo kisiochopungua miezi
sita..
Taarifa hii imetolewa baada ya kuonekana kushamiri vitendo vya kuvunja taratibu za usalama za usafiri wa treni.
Aina
hii ya uvunjaji huo wa matumizi yasiyo salama mwaka jana Agosti 03,
2016 yalisababisha , mtu mmoja kupoteza maisha baada ya kugongwa na
geti la lango la kuingilia treni Stesheni. Marehemu alikuwa
akinining’inia nje ya behewa wakati wa treni ya Pugu majira ya jioni
ikiingia ndani ya eneo la kituo kikuu cha Dar es Salaam..
Uongozi
wa TRL umefafanua kuwa tofauti ya usafiri wa basi ni kwa vile kondakta
anaweza kusimamisha basi ili kumshusha mtu anayening’inia nje lakini
kwa treni jinsi ilivyo ndefu hilo haliwezekani kufanyika kirahisi.
.
Aidha
katika taarifa hiyo Uongozi uimetoa wito kwa wasafiri na wananchi
kwa jumla kufuata masharti ya usafiri wa treni za jiji hasa wale wanao
tumia treni ya iendayo Pugu. Ili kuepuka maafa na pia kuchukuliwa hatua
za kisheria ambazo zitasababisha mkosaji kufungwa jela..
Wakati
huo huo Kikosi cha Polisi Reli kimeanza operesheni ya kuwadhibiti
abiria ambao hawataki kufuata sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya
usafiri salama wa treni na hasa kwa kuning’inia nje ya mabehewa wakati
treni ikitembea. Aidha operesheni hiyo itahusisha kuwafikisha mbele ya
sheria wasafri wote watakaokamatwa wakienda kinyume na masharti ya
usalama wa usafiri wa reli.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano:
Kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Ndugu Shaban Jumbe Kiko,
Mei 17, 2017
DAR ES SALAAM
SHARE
No comments:
Post a Comment