Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Onesmo Lyanga akizungumza jambo.(PICHA NA MWAMVUA MWINYI)
Na Mwamvua Mwinyi, Kibiti
HALI ya
sintofahamu bado inaendelea kutanda wilayani Kibiti ,mkoani Pwani ,baada
ya kutokea mauaji mengine ya kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi ,ndani ya
siku sita.Kaimu mkuu wa wilaya ya Kibiti ,Juma Njwayo ,alieleza
kwamba,mwenyekiti (CCM) tawi la Njianne ,kijiji cha Muyuyu ,ambae pia ni
mjumbe wa kamati ya siasa kata ya Mtunda ,Iddi Kilungi ,ameuawa kwa
kupigwa risasi.
Aidha
alisema , mtoto wa marehemu Nurdin Iddi Kilungi ,amenusurika kifo baada
ya kupigwa risasi ya tumbo na kutokea mgongoni.Njwayo ,alieleza
,majeruhi alikimbizwa hospital ya mission ya Mchukwi kwa ajili ya
matibabu.Alisema ,tukio hilo limetokea may 17 majira ya saa 1.40 usiku
wakati marehemu akiwa amejipumzisha kimazungumzo nyumbani kwake .
Kaimu
huyo ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Rufiji,Njwayo, alibainisha,watu
wawili wanaodaiwa kuwa ni wauaji walifika eneo la nyumbani kwa Kilungi
na kumpiga risasi na baadae kumpiga mwanae kisha kutokomea
kusikojulikana.Alisema watu hao waliegesha pikipiki mbali ya nyumba na
baada ya tukio walitokomea nayo .Kwa mujibu wa Njwayo, amemuagiza
mkurugenzi wa halmashauri ya Kibiti kumhamisha majeruhi (Nurdin
Kilungi)kwenda hospital ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu zaidi
.Alipoulizwa matukio hayo kuhusiana na masuala ya kisiasa alisema hawezi
kulisemea moja kwa moja jambo hilo kwasasa.Siwezi kujua kama ndio
chanzo ,mambo haya yanaendelea kuchunguzwa na vyombo vyetu vya kiusalama
,endapo itabainika basi umma utatangaziwa lolote lililopo lakini sio
kuhisi”alisema Njwayo.Kuhusiana na madai ya askari doria na kikosi
maalum kilichopo Rufiji,Kibiti kutoingia maeneo ya vijijini ambako ndio
kuna athari kubwa ,Njwayo,alieleza ,anachojua yeye ni kwamba kuna askari
wanaovaa sare na wasiovaa sare ambao wanafika mijini na
vijijini.Kamanda wa polisi mkoani Pwani,Onesmo Lyanga ,alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kudai ni siku sita tangu kutokea kwa mauaji
mnamo may 13 mwaka huu,ambapo katibu wa CCM kata ya Bungu ,Halife Mtulia
,aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
Alisema
chanzo cha mauaji hayo bado hakijajulikana kwani vyombo vya dola bado
vinafanya upelelezi ili kubaini kiini halisi cha matukio hayo ya mauaji .
Kamanda huyo alisema wanaendelea kuwasaka wahusika wa matukio hayo yanayoonekana kuhusisha viongozi mbalimbali na askari polisi.
Kamanda Lyanga ,aliwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kwa kufichua wahalifu ambao wapo miongoni mwao pasipo kuogopa .
Ni wazi
kwamba wahalifu wanaofanya mauaji haya wana wenyeji wanaowakumbatia kwa
kuwaficha hivyo yeyote atakaebainika kushirikiana na makundi ya uhalifu
huo atachukuliwa hatua kali za kisheria”alisisitiza kamanda Lyanga.
SHARE
No comments:
Post a Comment