Mwanafunzi mmoja
nchini Iran amelazimika kupelekwa katika kituo cha polisi mwishoni mwa
wiki iliyopita kisa na mkasa! Kufanana kulikokithiri na Lionel Messi.
Mkanganyiko huo ulianza miezi michache iliyopita wakati ba a wa kijana huyo aliyefanana mno na Messi alipompiga picha akiwa amevalia fulana ya timu ya Barcelona yenye namba kumi.
Reza Parastesh, ana umri wa miaka ishirini na mitano kwa sasa, hivi karibuni alianzisha mtindo wa ukataji nywele na kupunguza ndevu zake mithili ya mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Argentina.
Reza Parastesh, kwa sasa amebatizwa jina 'Messi wa
Iran' amejikuta kila wakati na kila mahali akiombwa kupiga picha na watu
wa aina kwa aina katika mji wa nyumbani kwao Hameden, nchini Iran.
Kijana huyo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kwa sasa watu watu wananiona mimi kuwa ndiye Messi wa Iran na kunitaka nifanye kiila kitu afanyacho Messi halisi, na pindi ninapotokeza mahali, watu hupatwa na mshtuko.
Nina furaha kubwa kuona kwamba ninawapa furaha na hili linapotokea linanipa ari mpya. Parastesh a.k.a Messi amekuwa ni mtu mwenye kufanyiwa mahojiano ya mara kwa mara na vituo vya habari na kufanikiwa kusaini mikataba mikubwa ya uoneshaji mavazi, na sasa ana fanya mazoezi makubwa ya kujua mbinu za mbira wa miguu ili akidhi vigezo wa Messi halisi.

SHARE
No comments:
Post a Comment