Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (wa pili kushoto) akisalimiana na
Viongozi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera katika ziara
yake mkoani humo kuzungumzia operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo
ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo
iliyotaifishwa kisheria na mahakama. Anayeongoza utambulisho huo
(kushoto) ni Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa
mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha
minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa
huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba,
Deodatus Kinawiro.
NA HAMZA TEMBA - WMU
---------------------------------------------------------
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe ameupongeza uongozi wa
Mkoa wa Kagera unaongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Meja Jenerali Mst. Salum
Kijuu kwa kufanikisha operesheni ya kuondoa mifugo katika maeneo ya
hifadhi mkoani humo huku akitoa tahadhari kwa watumishi wa hifadhi hizo
kupoteza ajira zao endapo wataruhusu mifugo hiyo kurudi tena katika
hifadhi hizo.
Ametoa
pongezi na tahadhari hiyo jana mjini Bukoba wakati akizungumza na
uongozi wa mkoa huo na kusema kuwa, kazi hiyo ni ya kupongezwa sana
kwakua imeleta matumaini ya uhifadhi mkoani Kagera na taifa kwa ujumla.
“Napenda
niwashukuru kipekee kabisa kwa jinsi ambavyo mlifanya ile operesheni ya
kuondoa mifugo kwenye hifadhi zetu, tulifanya kwa ueledi uliotukuka,
hata kama umesikia watu wanalalamika lakini hakuna aliyesema kuku wangu
waliuawa, walipigwa risasi, tulinyang’anywa mifugo, kazi hii ilifanywa
vizuri na kwa ueledi mkubwa sana”, alisema Prof. Maghembe.
Aliongeza,
“Hatutaruhusu tena mifugo hiyo irudi huko ndani ya hifadhi, hili ni
jambo kubwa ambalo ni wajibu wa wahifadhi wote kuhakikisha kwamba
hakuna mifugo itakayokuwa inaingia humo ndani, Kuanzia sasa kama
tutakuta mtu ameingia kwenye hifadhi yako wakati tunamuondoa tunamuondoa
yeye na wewe na familia yako yote ili mbegu yako mbaya isibaki katika
uhifadhi wa wanyamapori”.
Alisema
ili kuimarisha ulinzi katika hifadhi hizo, utaratibu wa kutumia ndege
maalum za doria na “drones” (ndege zisizo na rubani) utawekwa ili
kuwabaini wahalifu watakaokuwa wamekaidia agizo hilo ili wachukuliwe
hatua za kisheria.
“Tutakua
tunarusha ndege mara moja kila baada ya wiki tatu au wiki mbili
kuhakikisha kwamba hakuna mtu anaingia na mifugo humo ndani, lakini pili
tutafanya doria na ndege zile ambazo hazina marobani kuhakikisha kwamba
tunaangalia kinachotokea humo ndani wakati wote.
“Najua
wanaweza kubadilisha “system” (utaratibu) ikawa ya usiku na hawa askari
hawa tutawapa mafunzo maalum chini ya jeshi la wananchi wa Tanzania,
kuanzia miezi sita mpaka tisa, wajifunze namna ya kuhangaika na hawa
ambao wanaingia kwenye hifadhi zetu”, alisema.
Akizungumzia
operesheni hiyo, alisema ulitolewa muda maalum kwa watu kutoa mifugo
yao kwa hiari katika mapori ya akiba na hifadhi za misitu mkoani humo
ambapo wale wote waliotii hakuna mashtaka yeyote yalifunguliwa dhidi yao
ispokuwa wale waliokaidi walifikishwa mahakamani na mifugo yao
ikataifishwa kwa mujibu wa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori kifungu
namba 111 sehemu ya kwanza ambayo inaruhusu kutaifisha mali itakayokutwa
hifadhini.
Alisema
kuwa kumekuwepo na malalamiko mbalimbali juu ya utaratibu wa upigaji
mnada mifugo iliyotaifishwa ikiwemo minada hiyo kufanyika ndani ya
maeneo ya hifadhi, wenye mifugo kutoruhusiwa kuingia na wakati mwingine
kuwepo kwa malalamiko ya idadi tofauti ya mifugo iliyotaifishwa na
inayopelekwa mnadani.
Ili
kuondoa malalamiko hayo alielekeza kuwa baada ya amri ya mahakama
kutoka ni lazima mamlaka ya Wilaya husika ijulishwe na zoezi hilo
lifanyike katika maeneo ya wazi ili kila mwananchi anayehitaji aweze
kushiriki mnada husika.
“Minada
hii ifanywe kwa maelekezo ya mamlaka, hukumu ikitoka mkuu wa wilaya
ajulishwe, na kwamba mifugo kadhaa itapigwa mnada, na yeye ataamua mnada
ufanyike wapi na lini, na iwe sehemu ambayo kila mtu anaweza kufika,
minada hiyo iwe ya wazi na matangazo yatolewe ili malalamiko yasiwepo
ndio maana maelekezo yametoka minada isitishwe kwa muda wa siku saba
mambo haya yawekwe sawa”, alisema Maghembe.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu
alishukuru kwa ushirikiano alioupata kutoka Wizara ya Maliasili katika
kipindi chote cha utekelezaji wa operesheni hiyo ambayo amaeielezea kuwa
na mafanikio makubwa ikiwemo wanyamapori kuanza kurudi kwenye maeneo
yao katika Mapori ya Akiba ya Biharamulo Burigi na Kimisi.
“Niishukuru
wizara yako mmetupa ushirikiano mzuri, kule tumesafisha tumehakikisha
hakuna mifugo, hakuna kilimo, vitendo mbalimbali vya kibinadamu
vilivyokuwa vikifanywa kule vya kilimo, ukataji miti hovyo, kuchoma
mikaa, kulima mashamba mbalimbali ya mahindi, bangi, mirungi sasa hayapo
tena, Nashukuru kwa muda huu mfupi wanyama wengi wamesharudi, wengi
tuu, hadi Simba wamesharudi kwenye maeneo yao” alisema Kijuu.
Operesheni
ya kuondoa mifugo na wananchi waliovamia Hifadhi ya Misitu ya
Biharamulo, Nyantaka na Ruiga na Mapori ya Akiba ya Biharamulo, Burigi
na Kimisi mkoani Kagera ilianza tarehe 30 Machi, 2017 ambapo jumla ya
mifugo 5,939 ilikamatwa (Ng’ombe 5754, Mbuzi 140 na kondoo 45) na
watuhumiwa 185 walikamatwa na kufikishwa mahakamani.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba kuhusu operesheni ya kuondoa
mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha
minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa
huo, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus
Kinawiro (kulia), Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman (wa pili
kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander
Songorwa.
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akizungumza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba.
Picha
ya pamoja kati ya Waziri wa Maliasili na Utalii (katikati waliokaa),
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu (wa pili kulia
waliokaa), Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Deodatus
Kinawiro (wa pili kushoto waliokaa), Katibu Tawala Mkoa huo, Diwani
Athuman (kulia waliokaa), Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof.
Alexander Songorwa (kushoto waliokaa), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Laibooki (katikati
waliosima) na maofisa wa Mamlaka hizo.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mst. Salum Kijuu (kushoto) akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Laibooki (wa pili kushoto) Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo
(wa pili kulia) na Mkurugenzi wa Kudhibiti ujangili, Faustine Masalu
(kulia).
Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Prof. Alexander Songorwa (kulia), Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo (katikati) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania, Martin Laibooki (kushoto).
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akisalimiana na uongozi
wa Wilaya ya Biharamulo alipotembelea wilayani humo kwa
ajili ya kutoa maelekezo ya Serikali kuhusu operesheni ya kuondoa
mifugo katika maeneo ya hifadhi pamoja na taratibu sahihi za kuendesha
minada ya mifugo iliyokamatwa na kutaifishwa na mahakama. Anayeongoza
utambulisho huo (kulia) ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Sada Malunde.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza na viongozi wa Kamati
ya Ulinzi na usala ya Wilaya ya Biharalamulo na watumishi wa sekta ya
wanyamapori wilayani humo.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe akizungumza Kamati ya
Ulinzi na usala ya Wilaya ya Biharalamulo na watumishi wa sekta ya
wanyamapori wilayani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Sada Malunde na
Katibu Tawala Mkoa wa Kagera, Diwani Athuman (kushoto).
Baadhi ya askari na watumishi wa Idara ya Wanyamapori wa Wilaya ya Biharamulo.
Picha
ya pamoja ya Waziri wa Maliasili na Utalii, viongozi wa mamlaka za
uhifadhi, watumishi na kamati ya ulinzi na usala ya Wilaya.
Waziri
wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe akiagana na Katibu Tawala Mkoa wa
Kagera, Diwani Athuman pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali
wa Wilaya ya Biharamulo baada ya kumaliza ziara yake Mkoani humo ya
kujadili operesheni ya kuondoa mifugo kwenye maeneo ya hifadhi pamoja na
taratibu sahihi za kuendesha minada ya mifugo iliyotaifishwa kisheria.
SHARE
No comments:
Post a Comment