Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akiwasilisha
Makadirio ya Mapato na Matumizi (Bajeti) ya Wizara yake ya zaidi ya
shilingi trilioni 11.757, Bungeni Mjini Dodoma ili iweze kutekeleza
majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9 yaliyo
chini ya Wizara hiyo.

Viongozi
waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake,
wakifuatilia kwa makini Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo, Bungeni Mjini
Dodoma, ambapo kiasi cha shilingi trilioni 11.757 kimeombwa ili Wizara
hiyo iweze kutekeleza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa
mwaka wa Fedha 2017/2018.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa
akimpongeza Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), kwa uwasilishaji makini wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwenye
viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban,
akimpongeza Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango
(Mb), kwa uwasilishaji makini wa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo kwenye
viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Mhe. Peter Serukamba, mara baada ya Waziri Mpango
kuwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni Mjini Dodoma ambapo ameliomba
Bunge liidhinishe makadirio ya Mapato na Matumizi ya shilingi trilioni
11.757 ya Wizara hiyo.
Waziri wa
Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akisalimiana na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Prof. Juma Assad, kwenye
viwanja vya Bunge Mjini Dodoma.
Manaibu
Katibu wakuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Khamis Shaaban, na
Bi. Dorothy Mwanyika, wakibadilishana mawazo nje ya Ukumbi wa Bunge
Mjini Dododma mara baada ya kuwasilishwa kwa Bajeti ya Wizara hiyo
ambapo kiasi cha shilingi trilioni 11.757 zinatarajiwa kukusanywa na
kutumiwa na Wizara ya Fedha na Mipango.
Viongozi
waandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake, wakiwa
katika picha ya pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip
Isdor Mpango (wa tano kushoto), nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya
kuwasilishwa kwa Hotuba ya Bajeti ya Wizara hiyo. (Picha zote na
…………………………..
Benny Mwaipaja, WFM-Dodoma
Wizara ya
Fedha na Mipango imeliomba Bunge iidhinishie makadirio ya mapato na
matumizi (Bajeti) ya zaidi ya shilingi trilioni 11.757 ili iweze
kutekeleza majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2017/2018, kwa mafungu yote 9
yaliyochini ya Wizara hiyo.
Maombi
hayo yametolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango,
wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizaya hiyo,
Bungeni Mjini Dodoma, leo.
Dkt.
Mpango amesema kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 10.328 ni kwa
ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.429 ni kwa ajili ya
matumizi ya maendeleo.
Amefafanua
kuwa Matumizi ya Kawaida yanajumuisha shilingi bilioni 87.996 kwa ajili
ya mishahara, shilingi bilioni 778.612 kwa ajili ya matumizi Mengineyo
(OC) na shilingi trilioni 9.461 ni kwa ajili ya kulipa Deni la Taifa na
Huduma nyingine.
Aidha,
katika fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi trilioni 1.382 ni fedha
za ndani na shilingi bilioni 46.108 ni fedha za nje.
SHARE
No comments:
Post a Comment