TRA

TRA

Wednesday, May 24, 2017

Magufuli atikisa vigogo, Muhongo njia panda

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


RIPOTI ya mchanga wa madini kusafirishwa nje ya nchi umetikisa Taifa baada ya kuonekana kugusa vigogo wengi wa sekta hiyo serikalini.

Tayari Rais John Magufuli amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ajipime, ajitathmini na hatimaye aachie ngazi haraka.


Rais John Magufuli
     Prof Muhongo




Sababu kubwa ya kumtaka waziri huyo kufanya hivyo ni kutokana na kutokuwa makini kusimamia mchanga uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi hivyo kusababishia nchi kupoteza mabilioni ya shilingi.

Rais Magufuli alitoa maagizo hayo baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi ya mchanga huo kutoka kwa Tume aliyoiunda Machi mwaka huu.

Pamona na hayo, Magufuli alivunja pia Bodi ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na kumfukuza kazi, Mkurugenzi Mtendaji wa TMAA na kuwasimamisha kazi watendaji wa bodi hiyo kuanzia leo.

Aliagiza vyombo vya dola kuwafanyia uchunguzi watendaji hao waliokuwa wanahusika na kutathmini thamani ya mchanga wa madini uliokuwa unasafirishwa nje na wote wafikishwe kwenye vyombo vya dola.

Pia ameagiza aliyekuwa Kamishna wa Madini, aliyekuwpo wizarani hapo miaka minne iliyopita, akamatwe na kuchunguzwa na hatimaye kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Tume hiyo imebaini katika makontena ya mchanga 277 yaliyopo bandarini yana madini ya aina mbalimbali yanayofikia thamani ya sh. trilioni 1.4.  


Na J. J. MSACKY

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger