Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi ametoa siri ya uimara wa timu
ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 akisema: “Haya
yote kayafanya Dk. Harrison Mwakyembe.”
Akizungumza mjini Libreville,
Malinzi amesema: “Ujumbe wa kuitakia kheri Serengeti Boys ulitolewa na
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo umeisukuma timu hiyo
kufanya vema.
“…Ndiyo, timu imekuwa ikijindaa
physical, lakini kupata neno la mzazi kutoka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Dk. John Magufuli
kupitia Waziri wa Michezo, Mheshimiwa Mwekyembe liliwatia nguvu vijana
kufanya vema na kuzuia Mali kuIshinda Serengeti.”
Vyombo vya habari vya hapa
Libreville, vimesema Serengeti Boys ni timu ya kuchungwa mara baada ya
matokeo ya jana dhidi ya Mabingwa watetezi – Mali ambayo pia ni makamu
bingwa katika Kombe la Dunia la FIFA kwa vijana chini ya miaka 17.
Vyombo vya habari vya hapa
vimesema ni matokeo mazuri na hata ya kushangaza kwani Mali ni timu
ambayo hakuna timu inapenda kukutana nayo.
“La kushangaza kwa timu ya
Tanzania ambayo pamoja na Angola zina vijana wanaoonekana kuwa na umri
mdogo kulinganisha na timu za Afrika Magharibi, ni uwezo wao wa kubaki
kwenye mpango wa mchezo hata walipokumbana na mawimbi makali,” limesema
gazeti la Le Moniour.
Serengeti Boys imeanza
kufuatiliwa na kuangalia matokeo yake ya mechi za nyuma na kuonekana
imepoteza mechi chache za kimataifa na kuzifunga timu kama za Afrika
Kusini, kutoka sare na Korea Kusini na Marekani katika michuano
mbalimbali .
SHARE
No comments:
Post a Comment